KAMISHNA ATAJA SABABU YA KUIBUKA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI DAR ES SALAAM


Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar Es Salaam Idrisa Kayera akimkabidhi Hati mwananchi aliyepimiwa kipande cha ardhi.

Na Moses Mwakibolwa,Dar es Salaam

KAMISHNA msaidizi wa Ardhi mkoa wa Dar Es Salaam Idrisa Kayera amewataka wananchi kushiriki katika zoezi la upimaji linaloendelea katika wilaya mbalimbali katika mkoa huo na amesisitiza uwepo wa nyaraka muhimu wakati wa zoezi hilo hususani mikataba ya mauziano ardhi baina yao ili kurahisisha upimaji kufanyika kwa haraka na uhakika

Kayera amesema wakazi wa Dar Es Salaam wengi wanaishi katika maeneo ambayo hajapimwa na kupangwa katika utaratibu wa mipango miji, amesema zoezi hili limeanza kwa mafanikio makubwa sana kwa kuwa mpaka sasa mitaa mingi imeshatambuliwa na kupangwa,  kwa wananchi waliotimiza vigezo vya upimaji Hati zao hupatikana haraka bila usumbufu wowote

Mpaka sasa jumla ya mitaa 270 imetambuliwa katika zoezi la urasimishaji unakofanyika na tayari mitaa hiyo ipo katika hatua za kukamilika,

Kamishna amesema kuwa Wilaya ya Ilala ina mitaa 110, Kigamboni ina mitaa 19, Kinondoni ina mitaa 33, Temeke ina mitaa 44, Ubungo ina mitaa 64 amesema katika taratibu za mipango miji zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani zaidi ya vipande 604571 na tayari jumla ya  michoro 1998 imeshaandaliwa, na jumla ya  viwanja vilivyoainishwa ni 523353

Amesema wananchi wanapojitokeza kushiriki ni faida kwa pande zote mbili ambapo wananchi wanaweza kutumia Hati zao katika masuala mbalimbali nje ya utatuzi wa migogoro ikiwa ni pamoja na dhamana kwenye Taasisi za fedha pindi wanapohitaji mikopo

Kamishna huyo mesema gharama za upimaji zimepungua sana, haizidi asilimia 0.5  ambapo mwananchi yeyote anaweza kumudu gharama hizo, "wananchi wasiogope gharama, hili ni punguzo kubwa sana lililofanywa na serikali, ofisi zetu zipo wazi na kila mwenye swali anaweza kufika kuuliza kuhusu upimaji na umiliki wa Ardhi"

Jumla ya maombi 16000 yaliwasilishwa ofisi ya kamishna na tayari zaidi ya Hati 14000 zimekamilika na Hati 9818 zimeshachukuliwa na wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaam

Kayera amesema haya yote ni mafanikio ya Raisi wa awamu ya sita katika kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaam wanamiliki Hati kwa usalama wa miliki kwa wananchi na kuepuka usumbufu kama ilivyokuwa awali

Aidha mratibu wa urasimishaji mkoa wa Dar Es Salaam Laurent Mswami amesema wananchi wanatakiwa kuzitumia vizuri ofisi za manispaa zote kwa ajili ya kupata elimu ya umiliki ikiwa ni pamoja na faida zake kwani kutokapimiwa kuna madhara mengi ambayo yanaweza kujitokeza huko mbeleni

Mswami amesema asilimia kubwa ya wananchi hukosa fedha kwa ajili ya kulipia upimaji na kusababisha kuzorota kwa zoezi katika maeneo mbalimbali, amawataka wananchi kutumia fursa ya kupimiwa kwa muda mfupi sana tofauti na awali, kwani endapo kila kitu kikiwa tayari kwa maana ya nyaraka mtu hujipatia Hati ndani ya siku moja na endapo itazidi sana haizidi wiki moja

"Natoa rai kwa wananchi kushiriki zoezi la upimaji kwa faida yao, endapo utapima na kupata Hati zipo faida nyingi ambazo wananchi watazipata ikiwa ni pamoja na kuongeza vipato kupitia Taasisi za fedha" alisema na pia amewataka wananchi wote wa mkoa wa Dar Es Salaam wanaoishi kwenye maeneo yasiyo rasmi kuhakikisha wanaingia katika zoezi la urasimishaji ili kupata hati itakayowawezesha kiuchumi na kusisitiza kuwa suala hilo linafanyika kwa nia njema kwa nia ya kuwaongezea mtaji wananchi kwa kupatiwa nyaraka itakayowasiadia kukopa fedha benki
















Post a Comment

0 Comments

UDOSO SCHOLARSHIP FUND YAZINDULIWA