TAIFA GESI YAIPONGEZA TIC KUCHAGUA KAMPUNI NNE ZA NDANI KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI NA MAHIRI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), (Kushoto),akisaini mkataba wa makubaliano na moja ya kampuni yenye miradi ya kimkakati na mahiri ya Taifa Ges (Kulia),Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni  hiyo,Hamisi Ramadhani akitia saini ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi unaotekelezwa nchi nzima. 

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Taifa Gas, Hamisi Ramadhani  amekipongeza kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kuchagua kampuni nne za ndani ya nchi katika mikataba sita ya miradi ya kimkakati na mahiri kwa kuwa zinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa huduma,kibiashara na upatikanaji wa ajira kwa watanzania.

Akizungumza hivi karibuni jijini hapa  mara baada ya utilianaji saini wa mikataba ya miradi ya kimkakati Mkurugenzi huyo wa  Taifa Ges amesema kuchagua kampuni nne kati ya sita ndani ya nchi ni hatua kubwa ya na ni uzalendo uliofanywa na TIC.

Mkurugenzi huyo amesema hatua ya kutiliana saini  walikuwa wakiisubiri tangu mwaka 2017 kwa mara ya kwanza ilipoteuliwa.

Ramadhani ameongeza kwamba kampuni ya Taifa Ges, mwaka 2017 ilipata cheti na ngao maalumu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji
(EWURA), kwa uwekezaji mkubwa kutoka sekta ya gesi na 2019 kampuni hiyo ilizindua ghala kubwa hapa nchini  na ni mojawapo ya maghala makubwa  katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini ambalo lilizinduliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano marehemu John Magufuli.

Mkurugenzi huyo amekishukuru kituo cha uwekezaji TIC kwa namna kilivyoendesha mchakato wa kupata kampuni zeye vigezo vinavyotakiwa na vilivyoainishwa na kamati ya Taifa ya Uwekezaji ya (NICSO),katika mikataba sita ya miradi ya kimkakati na mahiri.

"Tulikuwa tunasubisi hatua hii ya kutiliana saini tangu mwaka 2017 kampuni yetu iliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa mwekezaji mahiri na tumerudi tena katika mchakato na hatimaye  kwa sasa tumetiliana saini  na TIC katika mikabata hii," amesema Mkurugenzi huyo. 

Amefafanua kuwa uchaguzi wa TIC katika kampuni hizo pamoja na kuangalia mbele wawekezaji watafanya nini pia wameangalia katika uwekezaji wa baadae ambapo kampuni hizo  zimejithibitishia dhahiri katika maeneo yao yanayowekeza na hayasubiri soko likue bali yanawekeza ili kupanua masoko.

Amesema kufanya vizuri katika sekta ya gesi ni hatua na kuamua kufanya uwekezaji wenye tija, kufikiria mikakati mikubwa bila kulalamika.


Post a Comment

0 Comments

UDOSO SCHOLARSHIP FUND YAZINDULIWA