MASHINE MPYA ZA KISASA ZA KUKUSANYIA MADUHULI YA JESHI LA POLISI ZAZINDULIWA



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini akizindua mashine ya kielektroni ya kukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na makosa  ya usalama barabarani (Kushoto),ni Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo, Christopher Kadio na wa pili (kulia),Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini akionesga mashine ya kielektroni ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na makosa ya usalama barabarani mara baada ya kuzindua.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAMILIKI na Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia na kufuata sheria za Usalama Barabarani pamoja na kulipa madeni wanaodaiwa bila kushurutishwa.

Hayo yamesemwa jijin Dodoma leo Aprili 27,2022, na Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini wakati akizindua Mashine mpya za kisasa za POS kwa ajili ya kukusunyia Maduhuli ya jeshi la polisi nchini  hususani katika kitengo cha usalama barabarani.

Amesema mashine hizo pia zitatumika  katika ununuzi wa silaha,Hati ya tabia njema pamoja  na kukusanyia tozo mbalimbali barabarani hususani kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani.

Sagini ameongeza kuwa Mashine hizo mpya zina tumia mfumo wa Androidi nankwamba ina Wireless ambayo  inaskani leseni,inauwezo wa kuchukua alama za Vidole pamoja na kupiga picha jambo ambalo litasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi yaliyokuwepo.

Pia Naibu Waziri huyo  amelipongeza Jeshi la polisi nchini kwa kutumia wataalamu wake wa ndani kuendeleza mfumo huo ambao unakwenda kupunguzia jeshi hilo malalamiko na kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao bila kutumia nguvu kubwa kwa kuwa mfumo huo.

"Mfumo huu kwa sasa unachukua taarifa  muhimu kwa dereva  na hawezi kuja kukataa kwa sababu alama za vidole havifanani dunia nzima.Nawapongeza  amini mfumo huu utakwenda kuwa chanya kwenu na kwa wananchi pia hatutegemei kupata malalamiko  ya kuwepo kwa makosa katika kumuandikia mtu kosa "amesema Sagini.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewataka watumiaji wa barabara hususani madareva kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano pale Askari wa usalama barabarani wanapotaka kuchukua taarifa zao kwa ajili ya kujiridhisha wanapoandika ama kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto.

"Kwa mashine hizi mpya inahitaji dereva achukuliwe alama za vidole,picha na kuskani leseni sasa niwaombe usiwe mbishi pale askari anapotaka taarifa hizi mtoe ushirikiano kikubwa tii sheria bila kushurutishwa"Amesema IGP Sirro.

Naye Mkuu wa kitengo cha TEHAMA (ICT) wa jeshi la polisi nchini ACP Dawson Msongaleli amesema kuwa mfumo huo ulianza kwa kufanyiwa majaribia kwa mkoa ya Dar es salaam na Pwani tangu mwaka 2017 baada ya kufanya kazi vizuri ambapo 2018 ukaanza kutumika kwa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Ameongeza  kuwa nia ya kutumia mashine hizo ni kuondokana na ule mfumo wa kujazana katika vituo vya polisi na kusababisha foleni isiyokuwa na maana na badala yake kila kitu kitafanyika kielektroniki.



Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU