MEI MOSI KULETA FURSA ZA KIUCHUMI DODOMA





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya mwenendo mzima wa sherehe za Mei Mosi kitaifa. 


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),kuwahamasisha wafanyakazi na wananchi kujitokeza.


Meneja Masoko wa benki ya CRDB Kanada ya Dodoma Jane Mapanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya kujipanga kwao katika utoaji wa huduma za kibenki.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

KATIKA kuelekea kilele cha sherehe za Maadhimisho ya wafanyakazi Mei Mosi Mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa sherehe hizo kitaifa na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan pia Mkoa huo leo umezindua hash tag ya #MEIMOSI2022dodomakivingine. 

Sherehe hizo zitaambatana na shughuli mbalimbali zikiwamo za maonyesho ya wajasiriamali pamoja na wakati, taasisi za Umma na huduma, wafanyabiashara wa Kati na wakubwa , taasisi za kifedha, Viwanda, vyama vya wafanyakazi, Wizara na wadau wengine katika  juma la Maadhimisho hayo kabla ya kilele hicho  ammbapo yatafanyika katika UKumbi wa Jakaya Kikwete Convention kuanzia Aprili 22 hadi 30 mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Aprili  14, 2022, jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema jana alikutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari lengo likiwa ni kuwashirikisha namna ya kuwa na kampuni ya hamasa ya sherehe za Mei Mosi ambapo kitaifa zitafanyika katika Mkoa huo.

Mtaka ameongeza kuwa Mkoa huo unashirikiana  kwa ukaribu katika Maandalizi shughuli hizo na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),Chama kinachoratibu Maadhimisho hayo kwa mwaka huu (TALGWU), na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi na wa Wadau.

"Katika kufikia azma ya serikali ya kuhakikisha kila fursa inayojitokeza inachangia ujenzi wa uchumi imara, uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na wadau umeazimia kutumia fursa ya Mei Mosi kitaifa kuziunganisha sekta zote za kiuchumi kwa manufaa mapana ya Taifa," amesema Mtaka.

Mtaka ameeleza kuwa katika  kuwakumbusha wananchi kauli mbalimbali za viongozi wakuu wa Mkoa umeendaa Nukuu za viongozi. Nukuu hizo zilitolewa katika Maadhimisho ya Mei Mosi na zitakuwa zikitoka kila siku kupitia vyombo vya habari ambayo ni # MEIMOSI2022dodomakivingine.

Naye Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amewataka wafanyabishara na wajasiriamali kutumia fursa ya sherehe za Mei Mosi kuonyesha biashara zao.

Aidha anewataka wafanyakazi kuhudhuria  wakati  wa maadhimisho hayo ili kutimiza malengo na kutaka sherehe hizo ziambatane na shughuli za maendeleo na watu.

"Nitumie nafasi hii kuwakumbusha wafanyakazi kushiriki kikamilifu akatika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza hivi karibuni, wafanyakazi pia mnapaswa kutumia fursa hii kuwashawishi watu wengine  kuwa na utayari wa kuhesabiwa,"alisisitiza. Na kuongeza kuwa.

Nawakarabisha wananchi, wafanyabishara na wajasiriamali kutumia fursa ya sherehe hizi kwani Mei Mosi  hii ni ya kifursa kupitia maonyesho haya," amesema.

Kwa upande wa wake Meneja Masoko  wa benki ya CRDB Kanada ya Dodoma Jane Maganga amesema kuwa katika maonyesho hayo watatoa huduma za kifedha na kwamba wamejiandaa vizuri kutoa huduma za kifedha.

" Tuna toa shukurani zetu kwa serikali ya Mkoa  wa Dodoma kwa kutupatia fursa hii ya kuifanya CRDB kuwa mdhamini mkuu katika shughuli hizi hivyo tunaahidi kutoa huduma zilizobora za kifedha," amesema Jane.

Ameongeza kuwa benki hiyo imeboresha huduma zake na kupitia Mei Mosi wananchi wataendelea kufahamu benki kwa ukubwa wake na kwamba huduma zote za mikopo zitatolewa.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU