Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel akiangalia eneo ambalo uongozi wa kijiji cha Haubi umetoa kwaajili ya ujenzi wa Mahakama.
Na Mwandishii wetu, Kondoa
MAHAKAMA ya Tanzania imesema katika mpango mkakati wa awamu ya pili wa maboresho ya Mahakama nchini ambao ulianza 2020 hadi 2025 inatarajia kujenga Mahakama 10 za mwanzo za mfano katika maeneo ambayo ilikuwa ni vigumu wananchi kufikia haki.
Haya yamesemwa jana wilayani Kondoa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kati ya Mahamaka hizo mbili zitajengwa Dodoma katika Kijiji Cha Kinusi wilaya ya Mpwapwa na Haubi Wilaya ya Kondoa.
Amesema Mahakama inaendelea na maboresho ambapo kwa mujibu wa mpango mkakati ulioanza tangu mwaka 2015 hadi 2020 ambapo mambo makubwa yamefanyika.
“Sasa tupo katika mpango mkakati wa awamu ya pili ambao umeanza 2020 hadi 2025, katika mpango mkakati huu kutakuwa na maboresho kwani hadi sasa Tanzania kuna Mahakama za mwanzo 960 huku mahitaji yakiwa ni 3900 hivyo bado kuna upungufu,”alisema.
Ameongeza kuwa:”Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamisi Juma katika vikao vyetu alielekeza kuwa ni vyema kuangalia namna ya kujenga mahakama za mwanzo kwa kuzingatia maeneo yasiyo pungua 10 ambayo ni vigumu wananchi kufikia haki na lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha haki inapatikana kwa urahisi.
0 Comments