Waziri wa Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wake na wafanyakazi wa wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Jimy Yonazi akizungumza wakati wa mkutano wa Wizara hiyo Nape Nnauye (hayupo pichani), na wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), tawi la Wiaara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Laurencia Masigo akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye.
Daktari wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa jiji la Dodoma Revocatus Baltazar akitia mada kuhusu magonjwa hayo katika mkutano wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nnauye ( hayupo pichani), na wafanyakazi wa wizara hiyo.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amasema kuwa wizara hiyo ina jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi na kuhakikisha inalipeleka Taifa katika mabadiliko ya dunia ya kidigitali.
Pia amezitaka Idara zinazosimamia miradi ya kitaifa inayotekelezwa kupitia wizara hiyo kuhakikisha inawajengea uwezo watumishi wote kuhusu mpango wa Taifa wa mawasiliano, Mfumo wa Anwani za makazi na Miradi ya Tanzania ya kidigitali kwa lengo la kuifahamu miradi hiyo ili wawe mabalozi wazuri kwa wadau wa nje ya wizara hiyo
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Nape katika kikao chake na wafanyakazi wa wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo lake alilolitoa wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya habari.
Amesema kuwa anajisikia fahari kufanya kazi na wafanyakazi hao na kwamba kila mmoja ajiaikie ni sehemu ya familia ya Wizara hiyo ya habari.
"Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kunipa wizara hii muhimu katika maendeleo ya nchi yetu," amesema Waziri huyo.
Waziri huyo amesema kuwa sifa nyingi ambazo wanapewa ni kwa sababu wafanyakazi hao wanafanya kazi kwa ueledi na kwamba wanahitaji kusifiwa.
Ameongeza kuwa wizara hiyo bado ni ndogo ambayo imeungabishwa hivyo wanawajibu wa kuitengeneza kwa kuwa wenzao walikuwepo walikuwa na mapungufu, changamoto wao watayarekebisha mapungufu hayo.
" Kwa Katibu Mkuu natamani vikao kama hivi viwe vinafanyika kila tunapoenda Mei Mosi, pia natamini tuwe tunafanya bonanza ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza," amesema Waziri huyo.
Amesema kuwa haina maana kama wafanyakazi hao watakuwa wakifanya kazi bila kujali afya zao kwa magonjwa ambayo wameelezwa namna ya kuepukana nayo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Jimy Yonazi ameeleza kwamba ni wajibu wa wizara yake kutengeneza mazingira bora ya utendaji kazi wafanyakazi hao kwa lengo la kufarahi na kufanya kazi bila msongo wa mawazo.
0 Comments