Msimamizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya wazazi katika tawi la Michungwani lililopo kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Godfrey Chilongola alifafanua jambo mara baada ya kutangaza matokeo.
Baadhi ya wanachama wa tawi la Michungwani lililopo kata ya Saranga Wilaya Ubungo waliojitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi leo Mei 21,2022 Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
WAGOMBEA wa Jumuiya ya wazazi waliochaguliwa kwenye nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo katika Tawi la Michingwani lililopo Kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo wametakiwa kushirikaiana ili kuendelea kukiimarisha
Chama Cha Mapindizi (CCM),na kuweza kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake.
Hayo yamesemwa leo Mei 21,2022 jijini Dar es salaam na Msimamizi wa Uchaguzi katika tawi hilo Godfrey Chilongola mara baada ya kutangaza matokeo, amesema CCM ni chama kikubwa na kwamba wagombea hao waoneshe uadilifu wao katika kutimiza majukumu yao.
Amesema jumuiya ya wazazi hasa nafasi ya mwenyekiti ndiyo moyo wa chama hicho hivyo anapaswa kufanya kazi kwa kujituma ili kuendana na kazi Rais Samia ambaye anaupiga mwingi kila sekta.
Msimamizi huyo ameeleza kuwa uchaguzi ulikuwa ni wa haki na mzuri hivyo wagombea waliochaguliwa wafanye kazi kwa kushirikiana.
" Viongozi wote waliochaguliwa leo na kamati ya utekelezaji waendelee kuchapa kazi ili wamsaidie mama Rais Samia kutendaji kazi," amesema Msimamizi huyo.
Awali akitangaza matokeo ya uchaguzi huo wa Jumuiya ya Wazazi msimamizi huyo amemtangaza Asha Mwakyonde kuwa mwenyekiti kwa kupata kura 38 za ndiyo na za hapana kura 2 Kati kura 40 zilizopigwa huku nafasi ya katibu ikichukuliwa na Hawa Kahindi ambaye amepata kura 39 na ya hapana 1 kati ya kura hizo na nafasi ya EMMA tawi imeenda kwa Nazareth Abelly ambaye amepata kura zote 40 za ndiyo.
Akizungumzia ushindi huo Mwenyekiti Asha Mwakyonde amewashukuru wanachama wa tawi hilo waliomchagua kwa kura nyingi huku akiahidi kushirikiana vema na chama hicho.
"Demokrasia imetumika vizuri, na haki pia imetendeka nilijiamini kiasi kwani nilikuwa na mpinzani wangi anaitwa 'Hapana' nilikuwa najiuliza je hapana akipata kura nusu itakuaje?. Kwa kweli nawashukuru sana Wanamichungwani haya sio mapenzi ni mahaba waliyonionesha nawaahidi kuwafanyia kazi," amesema Mwakyonde.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Tawi la hilo Zili Mghamba amewapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa na kuwataka waendelee kuijenga jumuiya hiyo.
'Uchaguzi umeenda vizuri ulikuwa na uhuru na haki wagombea walipata wasaa wa kuzungumza na wapiga kura nao walipata wasaa wa kuuliza wagombea maswali ma 3 na wagombea wakajibu vizuri," Mghamba.
0 Comments