Profesa Anna Tibaijuka akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la Walaka wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Na Asha Mwakyonde
WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),imesema kuwa inatoa elimu ili Watanzania waweze kuelewa namna ya kuandaa nafaka zinazofikia viwango ambayo wakala hiyo inavinunua.
Pia NFRA inatoa elimu kwa Watanzania wapate uelewa wa matumizi bora ya viuatilifu ili wasipate madhara kwa afya zao.
Akizungimza Julai 9,2022 katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Afisa Masoko Mkuu wa NFRA, Simon Bikaru amesema kuwa banda lao lina sehemu tatu za namna wanavyoandaa nafaka na kuhifadhi chakula pamoja na mradi wao mpya.
Amesema kuwa sehemu ya kwanza wanavyoandaa na kuhakikisha nafaka inakuwa na vigezo vyenye ubora na kwamba kuna sehemu za awali ambazo ndio zinaandaa nafaka namna wanavyovifikia vigezo na viwango.
Bikaru ameongeza kuwa sehemu nyingine ni hifadh ya asili ambayo imegawanyika katika sehemu mbili ya kupanga tofali na Ile ya maghala.
" Pia kuna sehemu ya pili ya uhifadhi kutumia viwatilifu hivyo tunataka kuwaeleza Watanzania namna bora ya kuandaa maghala yao na nafaka zao," amesema.
Ameeleza kuwa sehemu ya mradi umekuwa ni mkombozi kwao kwani umekuja kupunguza gharama na kuongeza ubora wa nafaka.
Awali Afisa Uhusiano wa NFRA Angela Shagali ameeleza kuwa taasisi hiyo ni ya Umma ambayo ipo chini ya Wizara ya Kilimo ikiwa na lengo la kuhakikisha usalama wa chakula nchini ili kukabiliana na upungufu wa chakula kwa njia ya kununua, kuhifadhi na kutoa chakula pale kinapohitajika kwa kuzingatia ufanisi na tija.
"Taasisi hii ipo katika Kanda nane ambazo ni Kipawa, Arusha, Makambako, Songwe,Songea, Sumbawanga, Shinyanga na Dodoma," amesema.
Ameongeza Kanda hizo ni za kimkakati zipo katika maeneo ya uzalishaji mdogo na mkubwa.
0 Comments