TBS YATOA UTARATIBU WA UKAGUZI MAGARI 'USED' KABLA YA KUFIKA NCHINI

Meneja wa Usimamizi wa Shehena zote zinazoingia nchini Mhandisi Saidi Mkwawa Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Na Asha Mwakyonde

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limesema kuwa  kuanzia Leo Julai 20 mwaka huu magari yote yaliyotumika ( Used motor Vehicles),yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanagaguliwa nchini humo kabla ya kuja Tanzania kwa utaratibu wa awali 

Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja wa Usimamizi wa Shehena zote zinazoingia nchini Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kuwa ukaguzi wa magari hayo nchini Japan utafanywa na kampuni ya EAA Limited ya nchini Japan kuanzia Julai 20 mwaka huu.

" Gharama ya ukaguzi utakaofanyika nchini Japan ni dola za kimarekani 150 kwa gari hivyo hakuna ongezeko lolote la gharama za ukaguzi, " amesema Mhandisi Mkwawa.

Amefafanua kuwa magari ambayo tayari yalikuwa yameshanunuliwa na yapo katika mchakato wa kusafirishwa au yalishapikiwa kwenye Meli kwa ajili ya kusafirishwa kuja hapa nchini  Tanzania kabla ya Julai 20 yatakaguliwa na TBS yatakapofika nchini bila adhabu yoyote.

Mhandisi Mkwawa amesema kuwa utaratibu wa kukagua magari kabla ya kuwasili nchini Pre- Shipment Verification on conformity to Standards ( PVoC), utasaidia kuepuka gharama za matengenezo kwa wanunuaji  wa magari.

Aidha ameeleza kuwa Shirika hilo linaendelea na  taratibu za kupata mawakala kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayotoka nchi za Uingereza, Dubai na Singapore na kwamba utaratibu wa nchi hizo utakapokamilika  waingizaji na wafanyabishara wa magari watapewa taarifa.


Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI