KIUMBA: TUTAKUWA NA SOKO LA UHAKIKA KWA CPB


Mkurugenzi wa kampuni ya MT and David, David Kiumba akifafanua jambo.

Na Asha Mwakyonde

MKURUGENZI  wa kampuni ya MT and David, inayojishughulisha na masuala ya uchakataji na uhifadhi wa mpunga pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mchele,  David Kiumba amesema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha kusaini mkataba wa kuuza mazao na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB), wanaamini uzalishaji wao mbali na kuwa mkubwa watakuwa na soko la uhakika.

Akizungimza katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara  ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yaliyofikia tamati Julia 13,2022 yaliyokuwa yakifanyika kwenye  viwanja vya  Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa Kiumba amesema zoezi hilo la kusaini mkataba na CPB limewapa nafasi kubwa katika mfumo wa utaendaji kazi kwa kuwa wanazalisha kwa kiwango kikubwa 

Kiumba ameeleza  kuwa Serikali imewapa kipaumbele na imewapa nafasi ya kufanya kazi na Bodi hiyo huku  akiahidi kufanya nao kazi vizuri na kuongeza ajira kwa vijana.

Ameongeza anafuraha kubwa ikilinganishwa na mwaka jana 2021 zaidi ya tani 200 zilikosa soko la uhakika kutokana na mzigo kuwa mkubwa sokoni.

" Kampuni yangu ipo wilayani Mbalali Mkoani Mbeya na tunaviwanda vitatu hivyo kupitia mkataba huu nitaongeza  ajira kwa vijana katika mazingira ya shughuli zangu pia uzalishaji utakuwa mkubwa na soko la uhakika, " amesema Mkurugenzi huyo.

Amesema awali hawakufahamu nini maana ya Bodi hiyo lakini baada ya kufafanuliwa na katika upande wa ununuzi malipo yao ni mazuri sio ya kucheleweshwa na kwamba dhamira yake ilikuwa ni kufanya kazi na serikali.




Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU