MOI YAPATA TUZO YA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA TIBA


Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango (Kulia),akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza kipengele cha utoaji huduma bora Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI),Dk. Respicious Boniface.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), (kati kati) ni  Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface  wakifurahia tuzo walioipata ya kipekee cha utoaji huduma bora katika banda lao.

Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), imeibuka mshindi wa kwanza kwa kupata tuzo kipengele cha utoaji huduma bora katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika yaliyofikia tamati jana yaliyokuwa yalifanyika katika viwanja vya  Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa.

Pia taasisi hiyo imewaona wagonjwa zaidi ya 500 tangu kuanza kwa maonyesho hayo hadi kufikia tamati jana wenye matatizo mbalimbali ambapo wengine walipewa rufaa kwenda MOI na wengine walifanyiwa mazoezi tiba na kupatiwa dawa katika maonyesho hayo.

Akizungimza Julai 13,2022 mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza kipengele cha utoaji huduma bora Msemaji wa MOI Patrick Mvungi amesema kuwa imekuwa heshima kwa taasisi hiyo kwa kuwa waandaaji wa maonyesho hayo pamoja na serikali wametambua kazi kubwa wanaoifanya na kuwapatia tuzo.

Mvungi amesema wanamshukuru kwa ushindi wa kwanza katika utoaji wa huduma bora.

" Tunashukuru Mungu maonyesho haya ya 46 yamefikia tamati na tumeweza kutangazwa mshindi wa kwanza kipengele cha utoaji wa huduma bora za tiba pamoja na utunzaji wa viungo saidizi," amesema.

Ameongeza kuwa Watanzania wameendendea kujitokeza kwa wingi katika banda lao tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho kupata huduma ambapo wamewaona wagonjwa zaidi ya 500 mbali na wale waliofika kutaka kujua huduma zao zinaendaje.

Mvungi amefafanua kuwa wagonjwa hao 500 waliofika katika banda lao walipata  huduma na wale ambao wanachangamoto ambazo zinataka huduma zaidi waliandikiwa rufaa ya kwenda MOI.

Amesema wangonjwa wengine waliofika katika banda hilo walipata huduma za  dawa bure na waliohitji mazoezi tiba walifanyiwa pale pale huku akisema hiyo ni sehemu ya mkakati wa MOI kuhakikisha huduma zinawafikia watu wa kipato cha chini.

" Hii ilikuwa ni fursa ya kipekee kwa watembeleaji wa maonyesho haya wameweza kupata huduma bure za kibingwa za mifupa, Ubongo, mgongo pamoja na mazoezi tiba. Tulikuwa na wataalamu wa lishe ambao nao walikuwa wakitoa elimu kuonyesha ni namna gani watu wanaweza kujiimarisha afya zao kupata lishe bora," amesema.

Aidha ameongeza kuwa mwitikio wa watu katika banda lao ulikuwa mkubwa wameweza kuhudumia wagonjwa wengi na wamefurahia huduma zao na kwamba hiyo ndio sababu ya wao kushinda.

Mvungi ameeleza kuwa wenye changamoto mbalimbali wameondoka katika maonyesho hayo lakini huduma zao zinaendelea MOI wafike kwani ni taasisi ya serikali na huduma zianatolewa kila siku.

Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI