TARI KIBAHA YATAJA MBEGU ZA VIAZI ZILIZOFANYIWA UTAFITI

Afisa Kilimo Kitengo cha Idara ya  Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha TARI Kibaha Flora Citungo akionyesha moja ya aina ya Miche ya mbegu za za viazi vitamu wanazozalisha.

Afisa kilimo Kitengo cha Idara ya Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha TARI Kibaha, Flora Citungo akionyesha moja ya Miche ya mbegu za za mihogo.

Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imesema kuna aina mbalimbali za mbegu za viazi ambazo zimefanyiwa utafiti na zimeruhusiwa kutumika kwa wakulima.

Pia akina mama wameshauriwa kutumia viazi lishe kwa kuwa vinasaidia kupata vitamini  A ambacho kinapatikana ndani ya kiazi na kwamba faida yake inawapunguzia tatizo la uoni hafifu.

Hayo yamesemwa Julai 10, 2022  katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere na Afisa Kilimo Kitengo cha Idara ya  Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha TARI Kibaha Flora Citungo amezitaja baadhi ya mbegu hizo zilizofanyiwa utafiti kuwa ni Mataya, Tari SP 3, Tari, SP 4, Tari, SP 5 ,Tari SP 6, Tari, SP 7 na Tari SP 8.

Amesema kuwa mbegu hizo zote zimefanyiwa utafiti na zimetuhusiwa kutumika kwa wakulima wa mazao ya viazi.

Afisa huyo ameeleza kuwa wana aina mbili ya  mbegu ya viazi vitamu na tayari imeshafanyiwa utafiti na kuruhusiwa kutumika kwa wakulima ikiwamo mbegu ya Simama. 

"Tuna aina za mbegu ya viazi vitamu ambayo ukiikata kata zinakuwa rangai ya maziwa. Tupo hapa kwenye maonyesho kuonyesha teknolojia mbalimbali inayohusu mazao ya mizizi hususan viazi vitamu na mihogo,"  amesema Flora.

Amefafanua kuwa kuna aina tatu za viazi vitamu ambavyo ni viazi vyenye rangi nyeupe, rangi ya chungwa au karoti na rangi ya maziwa.

Frola ameongeza kuwa kituo Cha kibaha wanahamasisha jamii kutumia viazi vyenye rangi ya  karoti kwa kuwa vimewekewa virutubisho vya vitamini A ambavyo vinasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Amefafanua kuwa viazi vitamu vinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali kama chapati, mkate na keki huku akisema kuwa viazi vyenye rangi karoti vinatumika kwenye mchanganyiko wa juisi ya matunda baada ya kuchemshwa na kusagwa.

Flora ameeleza kuwa majani ya viazi pia hutumika kama mboga na kiazi chenyewe kinaweza kutumika kama kiungo cha mboga kama karoti.

"Kilimo cha viazi vitamu kinalimwa sehemu zenye joto na baridi sehemu zanye joto kuanzia kupanda hadi kukomaa inachukua miezi 3 na kwenye baridi ni miezi 4," amesema.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU