WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUHAMASISHA ZOEZI LA SENSA

Afisa Masoko Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS),Andrew Punjila akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu uhamasishaji wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Na Asha Mwakyonde

OFISI ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imewaomba waandishi wa habari kupitia kalamu zao kuhamasisha Watanzania kuhusu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotajariwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu ambapo Maandalizi yake yamefikia zaidi ya asilimia 80.

Hayo yameyasema  Julai 11,2022 na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka NBS Andrew Punjila  katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere amesema waandishi wa habari ni watu muhimu na ni dataja kubwa katika kuisaidia serikali kufikisha ujumbe wa Sensa kwa wananchi.

"Tunaomba sana tusaidiane kuhamasisha wananchi ili  wawe na uelewa mkubwa kusudi itakapofika Agosti 23,mwaka huu wawe tayari kuhesabiwa na ni mara moja tu. Tunatumia fursa hii adhimu, majukwaa mbalimbali kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi," ameeleza Punjila.

Amesema kuwa lengo ni kupata uelewa kuhusu taarifa ambazo serikali inahitaji na kwamba watakusanya taarifa hizo za wanakaya wote kuanzia mkuu wa kaya  na wanakaya waliolala katika kaya husika.

Afisa huyo ameongeza kuwa mtu aliyelala tanzania atahesabiwa katika kaya aliyelala na kwamba kuna kaya maalumu kama vile nyumba za kulala wageni, vituo vya mabasi,uwanja wa ndege wote watahesabiwa mahali walipolala 

" Ni muhimu kwa wanakaya kuandaa taarifa za wanakaya watakaolala kwenye eneo husika. Hili ni zoezi muhimu litasaidia serikali kujua takwimu sahihi kwa kuwa inapambana na umasikini bila kujua idadi ya watu haiwezi kupanga, kukusanya tathimini ya miradi mbalimbali ya kuondoa umasikini hivyo taarifa zitasaidia," ameeleza.

Amewaomba viongozi wa dini, kimila, watu wenye ushawishi,wasanii  kuisaidia serikali katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili iweze kutimiza malengo yake 




Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU