TFRA YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA MBOLEA NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA),Dk. Stephan Ngailo akimsikiliza mteja aliyetembelea  banda la TFRA.

Na Asha Mwakyonde

WAWEKEZAJI wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuwekeza katika tasnia ya mbolea kwa kuwa fursa zipo nyingi kutokana na utashi wa kisiasa uliopo kwani mahitaji ya mbolea ni makubwa.

Akizungumza Julai 8,2022 katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA),Dk. Stephan Ngailo  amesema soko la mbolea ni kubwa hapa nchini na hata nchi zinazoizunguka Tanzania.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Tanzania ni kitovu cha mbolea katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

"Idadi ya watu inaongezeka na Ardhi inabaki pale pale lazima tuongeze tija kwa kuzingatia kanuni bora ikiwamo matumizi sahihi ya mbolea," amesema.

Akizungumzia maonyesho hayo Dk. Ngailo ameeleza kuwa lengo la kushiriki maonyesho ni kuchukua TFRA na kuipeleka kwa Umma waweze kuifahamu pamoja na majukumu yake na jukumu lake kubwa ni kusimamia tasnia ya mbolea zote zinazozalishwa hapa nchini na kuhakikisha zinakishi ubora na viwango vilivuowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kwa upande wake Kaimu Meneja Huduma za Sheria kutoka TFRA Belinda Kesi amesema wamekuwa wakihamasisha wadau wao kuzingatia matakwa ya kisheria.

"Kama mdau anataka kuingia katika tasnia ya mbolea ahakikishe anatambilika na Mamlaka husika kisheria, jukumu letu ni kusimamia tasnia hii pamoja na majukumu mengine," amesema

Ameongeza kuwa TFRA imeanzishwa mwaka chini ya Sheria Namba 9 ya mwaka 2009 ikiwa na jukumu la kusimamia tasnia ya mbolea nchini pamoja na majukumu mengine ni kuhakikisha mbolea hiyo inayotumika, inayoingia, inayosafirishwa nje ya nchi inakuwa katika ubora unaotakiwa na vigezo vya biashara vinazingatiwa.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA