TMDA:UTEKETEZAJI BIDHAA ZISIZOFAA KWA MATUMIZI WAONGEZEKA


Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 na matarajio ya mwaka 2022/ 2023.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imesema katika kipindi cha mwaka 2020/2021 kiasi na thamani ya bidhaa za dawa na  vifaa tiba visivyofaa kwa matumizi ya binadamu zilizoteketezwa zimeongezaka kutoka tani 14,704.80 zenye thamani ya shilingi bilioni 8.5 na kufikia jumla ya tani 35,547.47 zenye thamani bilioni 35.53 mwaka 2122.

Akizungimza Julai 29,2022, jijini hapa  kuhusu mafanikio ya Taasisi kwa kipindi cha mwaka 2021/ 2022 na matarajio ya mwaka 2022/2023, Mkurunzi Mkuu  wa Mamlaka hiyo Adam Fimbo amesema kuwa bidhaa hizo zinajumuisha zilizotolewa taarifa na zile zilizokamatwa katika kaguzi mbalimbali.

Mkurugenzi huyo amesema kuongezeka kwa bidhaa zilizoteketezwa kunatokana na kuimarisha ukaguzi na elimu kwa Umma inayosaidia wateja kutoa taarifa juu ya bidhaa zisizofaa kwa matumizi.

Akizungimzia udhibiti wa bidhaa za tumbaku ameeleza kuwa mamlaka hiyo iliandaa Mpango Mkakati Kazi wa miaka mitano 2021 hadi 2026 wa Kitaifa wa kupamabana na Tumbaku ambao tayari umeenza kutekelezwa.

"Tumeweka tayari mfumo wa udhibiti wa bidhaa hizi hadi sasa tumeshakwishatambua bidhaa zote za tumbaku zilizoko kwenye soko ambapo idadi yake hadi sasa ni bidhaa 51," amesema Mkurugenzi huyo.





Post a Comment

0 Comments

TANZANIA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA YA MAGARI YA UMEME SINGAPORE - DKT. BITEKO