FIMBO: TMDA IMEANZISHA MFUMO WA KIELEKTRONIKI UTOAJI TAARIFA ZA MADHARA

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),imeanzisha mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama ADR Reporting Tool wa utoaji wa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya Dawa kwa kutumia simu za mkononi, Kompyuta na kwa njia ya kutumia ujumbe mfupi kwenye simu.

Kupitia mfumo huo  TMDA  imepokea jumla ya taarifa 4,898 katika kipindi husika na hadi sasa taarifa hizo zimefika 31,666 kwenye mfumo wa taarifa unaosimamiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ujulikanao kama Vigibase.

TMDA ni Taasisi ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya Afya yenye jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, chanjo,vifaa tiba na vitendanishi pamoja na udhibiti wa bidhaa za tumbaku.

Akizungimza Julai 29,2022, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 na matarajio ya mwaka 2022/2023, amesema mamlaka hiyo imeweka mfumo madhubuti ya ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, chanjo na vifaa tiba kitaalam huitwa Vigilance System.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa lengo la mfumo huo ni kuweza kubaini, kutathmini na kuzuia madhara yasiyovumilika yasiyokee kwa wananchi pamoja na kuimarisha upatikanaji wa taarifa hizo.

"Taarifa hizi ni maudhui madogo ambayo hayapelekei kuondoa dawa kwenye soko," amesema Mkurugenzi huyo.

Mbali na hayo mkurugenzi huyo amezungumzia kuhusu Maabara za Mamlaka hiyo amesema TMDA ina maabara tatu zilizojengwa katika majiji ya Dar es Salam, Mwanza na Dodoma.

Ameongeza kuwa maabara hizo jukumu lake ni kufanya uchunguzi wa sampuli za bidhaa kwa lengo kujiridhisha katika ubora, usalama ili kuiwezesha mamlaka hiyo kufanya maamuzi ya kuidhibiti kabla ya kuruhusu au kutoruhusu bidhaa kutumika.

" Maabara ya kupima vifaa tiba kwenye maabara iliyoko Dar es Salaam imeimarishwa na vile vile maabara ya kupima bidhaa za tumbaku iliyopo Dodoma imewekewe Mitambo ya kisasa ya upimaji wa bidhaa hizi," amesema Fimbo.

Fimbo ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022 maabara hizo zimefanya uchunguzi wa  wa sampuli 1,808 za dawa vifaa tiba, vitendanishi na vipukusi  ambapo sampuli 1, 644 sawa na asilimia 91, zimefaulu.

Pia amefafanua kuwa kiwango cha ufaulu wa bidhaa zilizochunguzwa umeongezeka kutoka asilimia 88 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 91 mwaka 2021 na 2022.

" Hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa wadau na kuimarika kwa udhibiti wa bidhaa katika soko," amemema Fimbo.

Aidha ameeleza kuwa jumla ya sampuli 2,289 zilichunguzwa kupitia maabara hamishika kwenye vituo 25 nchini kwa lengo la kufanya uchunguzi wa awali wa dawa ambapo sampuli zote zilifaulu.

Post a Comment

0 Comments

TANZANIA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA YA MAGARI YA UMEME SINGAPORE - DKT. BITEKO