Na Mwandishi wetu, Arusha
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara,Dkt.Franklin Rwezimula ,ameipongeza Timu ya Wataalam ya Uandaaji Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara kwa kufanya mapitio ya nyaraka mbalimbali,kukusanya taarifa kwa kutembelea maeneo mbalimbali tanzania bara na zanzibar na kufanya majadiliano na taasisi za umma,asasi za kiraia pamoja na kutumia uzoefu kutoka katika nchi jirani ili kuweza kufanikisha kuandaa taarifa ya tathmini ya haki za binadamu ikiwa ni nyaraka muhimu katika uuandaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa majumuisho ya kikao cha Kamati ya usimamizi uuandaji wa Mpango huo kilichofanyika tarehe 14-15 Novemba,2024 Jijini Arusha.
Pia Dkt Franklin ametoa shukrani kwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) na wadau wengine kwakutoa ushirikiano na kufadhili katika hatua mbalimbali za Mchakato wa Uandaaji wa Mpango Kazi huo.
0 Comments