đź“ŤAsema Vikundi ambavyo havijafanya marejesho zaidi ya miezi miwili vimepewa notisi.
Na Asha Mwakyonde DODOMA
HALMASHAURI ya Mji Kondoa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imefanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali shughuli za kijamii zikiwamo Usajili wa vikundi.
Said Majaliwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa anazungumzia shughuli zilizofanywa na Halmashauri hiyo kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii katika taarifa ya baraza la madiwani la mwisho wa mwaka 2023/2024 anasema Idara ilifanikiwa kusajili jumla ya vikundi 16 na kupata hati za utambuzi.
Mkurugenzi huyo anafafanua kuwa vikundi vilivyopata hati ya utambuzi ni vya vijana ambavyo ni vitatu na vikundi vya wanawake 13 na kwamba hakuna kikundi cha watu wenye ulemavu kilichosajiliwa.
Anasema kuwa ufuatiliaji wa marejesho ya vikundi vilivyopatiwa mikopo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021,2021/2022 na 2022/2023 ufuatiliaji huo umefanyika kwa vikundi 30 ambapo zaidi ya Shilingi milioni 112 sawa asilimia 81 kati ya Shilingi milioni 138, zimerejeshwa.
"Vikundi ambavyo havijafanya marejesho ya fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa zaidi ya miezi miwili vimepewa notisi na kupelekwa mahakamani,"anaeleza Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mji Kondoa.
Anaongeza kuwa Halmashauri hiyo imefanya ufuatiliaji na ukaguzi kwa Taasisi za kifedha (Micro credits), na vikundi vya huduma ndogo za fedha na kwamba ufuatiliaji wa ukaguzi huo umefanyika kwa Taasisi hizo 19 na Vyama vya Akiba na Mikopo( SACCOS),mbili zinazojishughulisha na biashara ya huduma ndogo za fedha pamoja na kuweka na kukopa.
"Ukaguzi huo umefanyika kwa lengo la kukabiliana na mikopo chechefu inayoleta kero kwa wananchi na watumishi," anaeleza Majaliwa.
Aidha mkurugenzi huyo anasema kwamba vikundi vya huduma ndogo za fedha 34 vimefuatiliwa na kukaguliwa ili kuhakiki utekelezaji wa shughuli zao.
MFUKO WA AFYA YA JAMII (iCHF)
Majaliwa anaeleza Idara ya Maendeleo ya Jamii ilifanikiwa kufanya uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (iCHF), ambapo Kaya 466 zilisajiliwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 zenye makusanyo zaidi ya Shilingi millioni 13 na kuwekwa kwenye akaunti ya mfuko wa afya wa Mkoa wa Dodoma.
KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
Mkurugenzi huyo anasema Halmsahauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii ilifanikiwa kutoa elimu juu ya Ukatili wa kijinsia, VVU/UKIMWI, Ulawiti, Ubakaji, Ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni.
Anasema pia Halmashauri hiyo imefanikiwa ufuasi mzuri wa dawa na Matumizi sahihi ya Kondom, Jumla ya kondom 359,265.00 zimetolewa kwa mwaka 2023/2024.
0 Comments