DK. MPANGO: WAJASIRIAMALI WALIOFANIKIWA WAKATOE ELIMU VYUONI

Na Asha Mwakyonde, Mbeya

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amemtaka kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Wakili  Triphonia Kisiga,kama  ikiwezekana  wajasiriamali waliofanikiwa wahurisiwe kwenda  kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana waliopo vyuoni    namna walivyopata mitaji, walivyoanza ujasiriamali wao kwa lengo la kuhamasisha kundi la vijana hao  kujiunga na ujasiriamali badala ya kusubiri kuajiriwa.

Dk Mpango amesema hayo Agosti 1, 2022 wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya wakulima Nane Nane yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya amesema kuna baadhi ya wajasiriamali wamekuwa wakifanya mambo makubwa kwenye sekta hiyo.

Amesema kuwa  vijana wengi wanafikiria kuajiriwa pekeyake wakati   kwenye sekta ya  ujasiriamali kuna fursa za kujiajiri  ni vema wsjasiriamali wakaenda kuwafundisha vyuoni ili kuwatoa vijana hao katika dhana ya kusubiri ajira serikalini.

Amesema ujasiriamali kama huo,unapaswa kufanywa na vijana wanaohitimu vyuo ili waweze kupiga hatua kwenye kuinua uchumi lakini pia kuweza kujiajiri wso wenyewe katika maeneo mbalimbali ya ujasiriamali.

Hata hivyo ameitaka halmashauri ya mbeya ambayo baadhi ya mabanda ya mbegu walikuwepo humo,aliwataka kuwa na aina bora ya mbegu ambayo itamuwezesha mkulima kuitumia na kupata mazao bora.

Naye Waziri wa Kilimo Husein Bashe amesema serikali imeonyesha utayari wa kuwekeza kwenye sekta ya kilimo ambapo alisisitiza wakulima hawazi kukua bila kuheshimu sekta hiyo.

Waziri huyo meeleza bila kuwekeza katika sekta ya fedha tusingefikia hapa tulipo hivyo amewapongeza CRDB na NMB kutokana na kuweza kuelewa utoaji mikopo wa riba nafuu ikiwemo kuitekeleza.


"Benki ambazo hazitaelewa hili la mikopo ya rina nafuu hatutafanya nazo kazi,"alisema Bashe.

Katika hatua nyingine Waziri Bashe amesema baada maonyesho hayo makamu wa Rais atashuhudia utiaji saini wa mirafi yabilion 400 ya umwagiliaji ikiwemo kuzindua skimu za utoaji ruzuku za mbolea.

Pia amesema kuna tatizo kubwa la rumbesa kwa wakulima ma halmashauri zimegeuza hilo kama chanzo cha mapato.

Amemuomba Makamu wa Rais kukemea wakuu wa wilaya,mikoa na wakurugenzi kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia kama chanzo cha kujipatia mapato.

Post a Comment

0 Comments

WAZIRI SILAA AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO KATA YA MAKURU, SINGIDA