CPB YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA SOKO LA UHAKIKA


 Na Asha Mwakyonde,Mbeya

MKURUGENZI wa Bodi ya Nafaka ya Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi amesema amewahakikishia wakulima  soko la uhakika kutokana na Bodi hiyo kuendelea  kujenga viwanda vya kuchakata na kuyaongeza mnyororo wa thamani katika  mazao ya wakulima.

Pia amewataka wakulima ,wafanyabiashara kutembelea banda la CPB  kwa lengo la kujifunza na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa  katika mausala ya kilimo kupitia Bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wakulima na wafugaji (Nane Nane )yanayofanyika Kitaifa mkoani Mbeya, amesema Kwa sasa Bodi hiyo ina viwanda vinne hivyo wakulima watakuwa na soko uhakika katika mazao yao wanayozalisha.

Amesema,kutokana na viwanda hivyo ,Bodi hiyo inanunua mazao ya wakulima na kuyaongeza thamani na kuyauza ndani na nje ya nchi.

 “Tupo katika maonyesho haya kwa ajili ya kutambulisha wakulima bidhaa zetu lakini pia kuwafahamisha wananchi huduma zinazotolewa na CPB.

Mkurugenzi huyo amesema,malengo yao ni  kupata viwanda vingi zaidi ili kuwafikia wakulima wote na kuwafanya kuwa na uhakika wa masoko ya kuuza mazao yao. 

Mkurugenzi huyo Pia amesema,njia nyingine ya wakulima kupata masoko ya uhakika ni kwa kutumia mtandao mpana wa CPB ambao upo ndani ya nan chi. Kwa mujibu wa Dkt.Moshi ,mtandao huo wa masoko pia upo katika nchi zote za Afrika Mashariki pamoja na Asia na Ulaya ambapo CPB inaendelea kujenga uwezo huo wa kimtandao ili kupata masoko zaidi ya kuuza mazao ndani na nje ya nchi. 

“Tunataka wakulima na wadau wote wa tasnia ya kilimo wajue kwamba CPB inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafisha ,kuhifadhi,kupima mazao katika mikoa mbalimbali ikiwemo mikoa ya Arusha,Mwanza,Dodoma na Songwe.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA