FAHAMU UTAJIRI WA WILAYA YA TANGANYIKA


MKuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Halmashauri hiyo.

Na Asha Mwakyonde, Mbeya

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika ilivyopo mkoani Katavi, Onesmo Buswelu amesema kuwa wanakilimo ambacho kinawezeshwa na uwepo mifugo pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Hayo ameyasema Agosti 2, 2022 katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu Nane ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale amesema Wilaya hiyo imebeba historia ya nchi.

Amesema Wilaya ya Tanganyika imepakana na Wilya ya Uvinze Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Mpanda na pia imepakana na Ziwa Tanganyika.

"Kwa mbele tumepakana  na nchi ya DRC Kongo, Tanganyika imebeba historia ya nchi yetu tumeipatana Tanzania na Zanzibar kutoka Tanganyika," amesema Buswelu.

Ameongeza kuwa wapo katika maonesho hayo kuonyesha bidhaa zao kama mifugo na Teknolojia mbalimbali ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya mifugo na uvuvi ikiwamo kuimarisha na kuboresha maisha ya wananchi  wa Tanganyika kiuchumi.

Buswelu amefafanua kuwa Wilaya hiyo inazalisha chakula kwa wingi na kwamba ina  takriba zaidi ya tani  550,000 za chakula cha ziada  na kwamba hayo yote yametokana na uwezeshaji katika sekta ya kilimo ambapo Rais Samia Suluhu Hassan aliiwezesha katika mambo mbalimbali.

Ameeleza kuwa Wilaya hiyo imekuwa ikitembelewa na mawaziri mbalimbali na kutoa hamasa kwa wananchi katika masuala ya kilimo.

" Katika maonesho haya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imekuja na  wataalamu mbalimbali waliobobea katika mausala ya kilimo, wajasiriamali, wakulima  ambao wamekuja na bidhaa zao," amesema Buswelu.

Awali Mkurugenzi wa Wilaya ya Halmashauri ya Tanganyika Shabani Juma amewakaribisha wananchi wa Mbeya na maeneo ya karibu kutembelea banda la Halmashauri hiyo.

Juma amesema kuwa wanazalisha mazao ya biashara  na chakula huku akiyataja baadhi ya mazao hayo kuwa ni  pamba, kahawa,mshindi, alizeti,mihogo, mpunga, asali pamoja na ufugaji ukiwamo wa samaki.

" Nawakaribisha wananchi wa Mbeya kuja kujifunza na kujionea bidhaa tunazozalisha katika Halmashauri yetu ya Tanganyika, " amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha amewahamashisha wananchi kwenda kuwekeza kilimo cha biashara katika wilaya hiyo kwa kuwa Halmashauri ya Tanganyika ina maeneo yanafayofaa kwa kilimo hicho. 

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA