SAGCOT: SEKTA BINAFISI NDIO ZINAWEKEZA KATIKA KILIMO

 

Mkurungenzi Mtendaji wa Mpango wa  Kukuza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), 
Geoffrey Kirenga, akielezea mafuta ya Parachichi yanayozalisha na kampuni ya Olivado nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa kuuza Kilimo Ukanda wa Kusani mwa Tanzania (SAGCOT), akionyesha na kufafanua aina ya Parachichi linatumika kutengeneza mafuta ya Parachichi ambalo halifai kusafirishwa nje ya nchi.

NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

MKURUGENZI Mtendaji wa MPANGO wa  Kukuza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), 
Geoffrey Kirenga,  amesema kuwa sekta binafisi ni muhimu kwani ndio zinazowekaza katika kilimo huku akisema sehemu kubwa ya kazi ya uwezeshaji inafanywa na Taasisi za kiserikali.

Akizungimza  Agosti 2, 2022 katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu Nane yanayofanyika Kitaifa mkoani Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale Kirenga amesema kuwa ndani ya SAGCOT kuna  Wizara ya Kilimo kupitia taasisi za kiserikali ikiwamo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na sekta binafisi kama Baraza la Kilimo Tanzania (ACT).

"Kuna washiriki 60 katika  maaonesho haya wanaohusiana na kilimo, biashara, kusimamia kanuni na sheria  kati yao 30 ni wale wanaojihusisha na masuala ya uwezeshaji, kuongeza thamani vile vile kupeleka kwenye masoko," amesema Kirenga.

Kirenga amesema kuwa kazi inayofanyika na SAGCOT ni ya uratibu na kwamba wanafanya kazi moja kwa moja na wale wanaotoa huduma kwa wakulima kupitia vikundi na vyama vyao.

Akizungimzia ACT Mkurugenzi huyo amesema kuwa ni Baraza linalotoa huduma mbalimbali ili kuziwezesha sekta binafisi ziweze kupata huduma bora serikalini.

Pia Kirenga amesema kuna kampuni ya Olivado inafanya usindikaji wa mafuta ya Parachichi ambayo ilianzia nchini New Zealand, Kenya na baadae kuja Tanzania.

" Lengo la kuileta kampuni hii nchini kwetu ili watu wapate elimu na fursa za uwekezaji, wamewekeza takribani dola milioni 3 na wanaweza kufika dola milioni 5, wapo katika Mkoa wa Njombe," amesema Kirenga.

Amefafanua kuwa mafuta hayo yanatokana na maparachichi ambayo hayana sifa za kuuzwa katika masoko ya nje ya nchi Ulaya na Marekani.

Mkurugenzi huyo amesema katika msimu uliopita kampuni hiyo ilinunua Parachichi za shilingi milioni 500.

Kirenga amesema kuna uwezekano  milioni 500 hadi bilioni  3 kwa mwaka ambapo awali wakulima walikuwa hawazipati lakini kutokana na usindikaji huo mkubwa ambapo mafuta hayo yanauza nchini Marekani inatoa mchango wa kuingiza fedha za kigeni.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa lengo la SAGCOT ni ifikapo 2030 Tanzania iwe inauza bidhaa nje ya nchi zisizopungua fedha za kigeni dola bilioni 5 kwa mwaka.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya Olivado Tanzania Joseph Nkondola amesema kuwa mbali na kuzalisha mafuta hayo kampuni hiyo inachakata mabaki , taka taka na kuzatengeneza gesi ya Bio gesi.

"Tunatarajia pia taka taka zinazobaki tuweze kuzalisha mbolea ambayo itawasaidia wakulima," amesema Nkondola.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA