KAMISHNA MSAIDIZI SHILE: HUDUMA ZA IDARA YA UHAMIAJI NI BORA



NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA 

KAMISHNA Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, ambaye pia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Shigongo Shile amewaomba Watanzania kutumia huduma zinazotolewa katika banda la  Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji.

Pia amewaomba Watanzania kua tayari kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili serikali iweke mipango endelevu na bora kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Akizungimza Agosti 2, 2022 katika maonesho ya  kitaifa ya wakulima na wafugaji maarufu Nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale Jiji hapa amesema Idara hiyo inaawasaidia kuwapatia hati ya kusafiria nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wenzao ambao wapo nje ya nchi.

Amesema kuwa watanzania wataomba hati ya kusafiria huku akisema wageni watakaoingia nchini wataomba visa.

Kamishna huyo ameongeza kuwa Idara hiyo inatoa huduma hizo kwa mfumo wa kieletroniki huku akisisitiza kwamba huduma zao ni rafiki na ni bora 

"Idara hii inatekeleza majukumu makuu matatu ambayo ni uhamiaji, usalama na maendeleo.Jukumu la tatu ambalo ni la msingi la maendeleo linahusisha Idara ya Uhamiaji na wadau muhimu ambao wamewekeza katika sekta mbalimbali kwenye kilimo mifugo na uvuvi," amesema.

Amefafanua kuwa Watanzania ili wawe na shughuli zenye tija ni muhimu kubadilishana teknolojia, mawazo,mbinu na mikakati mbalimbali ya kuboresha shughuli zao.

Kamishina Shile ameeleza  hiyo inawawezesha Watanzania kutoka nje ya nchi kwenda kutafuta wenzao kwa ajili ya kubadilishana uzoefu au kupata teknolojia nyingine ili kuongeza thamani kwenye shughuli zao.

" Sisi kama Idara ya Uhamiaji ni wadau ambao tunashiriki katika maonesho haya. Nadhani mtajiuliza kwanini tunashiriki kama mnavyofahamu kaulimbiu ya mwaka huu inasema "Kilimo ni Biashara Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi" ili Watanzania wawe na kilimo bora na chenye tija ni muhimu kwao kuongeza thamani katika shughuli zao," amesema.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA