VETA YAJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KIFAA CHA KUKAUSHIA NGUO ZA NDANI


Mwalimu na Mbunifu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA ),Dar es Salaam Bukuku akiwaelezea baadhi ya watu waliotembelea banda lao kuhusu teknolojia ya kifaa cha kukaushia nguo za ndani kitakavyopunguza mangonjwa ya fangasi, ngozi na ya Urinary Tract Infection, U.T.I hasa kwa wanawake na watoto.

NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia chuo cha Ufundi Stadi cha Dar es Salaam kimebuni kifaa  cha kukaushia nguo za ndani kinachoitwa Dhydrator mashine lengo likiwa ni kupunguza, kutokomeza magonjwa yatokanayo na Fangasi, ya ngozi pamoja na Urinary Tract Infection, U.T.I.

Pia Watanzania wametakiwa kukubali teknolojia ambazo zinabuniwa na wazawa ili kuwapa hamasha ya kuongeza juhudi katika bunifu zao ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa wanazozibuni. 

Akizungimza  jijini Mbeya Agosti 3, 2022, katika  maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu Nane nane  yanayoendelea  viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika mkoani hapa  katika banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kutoka Chuo cha VETA Dar es Salaam  Mwalimu na Mbunifu kutoka Chuo hicho Emmanuel Bukuku ,amesema kuwa watanzania wanaamini bidhaa zinazotoka chini kuliko kuuamini zinazobuniwa nchini .

Mwalimu Bukuku amesema kuwa
Baada ya kuona changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani alikaa chini na kubuni mashine ambayo itaondoa changamoto hiyo ya kukausha nguo hizo kwa muda mfupi na mashine hiyo inatumia umeme kidogo 

Amesema kuwa nguo za ndani mara nyingi zikifuliwa huwa zinaanikwa ndani hali inayowasababishia watumiaji kupata magonjwa kutokana na kukuza wadudu ambao wanasababisha magonjwa kama Fangasi.

Kilichomsababishia kubuni mashine hiyo Mwalimu huyo amesema kuwa aliona jamii ina changamoto ya kupata magonjwa kama vile Fangasi, ya ngozi na U.T.I  kwa watu wazima na watoto hivyo kifaa hicho kitasaidia kupunguza magonjwa hayo au kuyatokomeza kabisha.

" Kwa upande wa afya  hii ni teknolojia nzuri na jamii bado haijajua hii mashine  kwa ubunifu huu tunaweza kuwakomboa watoto wengi wanaokumbana na magonjwa ya U.T.I na Fangasi, pamoja na wanawake hii inaweza kuwa mkombozi kwao,"ameongeza.

"Katika maonesho ya mwaka huu ya Nane nane tumeweza kuja na teknolojia mpya ya kifaa, mashine ya kukaushia nguo za ndani," amesema Mwalimu Bukuku.

Mwalimu Bukuku amefafanua kuwa mashine hiyo ametengeneza kwa muda wa wiki tatu na kuifanyia majaribio ambapo  ilionesha ipo vizuri na inauzwa kwa shilingi 350,000.

Amesema mashine ipo kama dressing table ambapo mtumiaji atanufanika na vitu viwili atatumia kukuangalia kupitia kioo na chini kukaushia nguo za ndani.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA