SERIKALI KUTUMIA BILIONI 8 KUSOMESHA MADAKTARI 457


  NA ASHA MWAKYONDE DODOOMA,

MADAKTARI 457 katika Ubobezi na Ubingwa wa magonjwa mbalimbali wamepatiwa ufadhili wa kusoma ambao utagharimu Shilingi bilioni 8 kwa mwaka 2022/2023 na kati yao 139 kusoma nje ya nchi.


Akizungumza Jijini hapa  leo Oktoba 28, 2022 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa

idadi hiyo madaktari 139 watasoma nje ya nchi, na madaktari watatu watasoma ndani ya nchi, mpango wa Rais Samia ni kuongeza wataalam wanaotoa huduma za kibingwa na ubobezi


Waziri Ummy amefafanua kuwa ufadhili huo utahusisha nauli,posho ya kujikimu na ada pindi watakapokuwa masomoni.


Aidha Waziri Ummy alitaja Hospitali zitakazonufaika na ufadhili huo ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo madaktari wake watasomea  ubingwa na ubobezi katika kupandikiza figo, uroto,vifaa vya kusikia na upasuaji wa kinywa na koo. 

Waziri Ummy amezitaja Hospitali nyingine itakayonufaika na ufadhili huo kuwa ni  Mloganzira ambayo itabobea katika mfumo wa upumuaji na Kiharusi wakati Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma itahusika na magonjwa wa Figo, Saratani na upandikizaji wa Uroto.

Aidha Waziri Ummy ameeleza kuwa  Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) itahusika na mishipa ya damu, uti wa mgongo  na huduma za mazoezi tiba na maradhi  ya ajali.

Waziri Ummy ameongeza kuwa  Hospitali ya KCMC Moshi itahusika na Ubingwa na ubobezi wa magon jwa ya Ngozi, mfumo wa mkojo wakati Bugando itahusika na huduma za Saratani.

Waziri huyo amesema kuwa Hospitali ya Ocean Road itahusika na ubingwa na ubobezi katika  tiba ya mionzi na upasuaji wa saratani.

Aidha Waziri Ummy amesema licha ya kupeleka madaktari hao nje lakini bado kuna changamoto ya madaktari Bingwa na ubobezi katika wa dawa ya usingizi, upasuaji wa ubongo, tiba ya mishipa ya fahamu.

Aidha Waziri Ummy Ameeleza, changamoto nyingi ni uhaba wa wataalam wa Afya ya akili, tiba ya kinywa na koo.

Hata Waziri Ummy amesema, madaktari hao watakaoenda masomoni wapewa masharti wakimaliza hawataruhusiwa kufanya kazi sehemu yoyote zaidi ya Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha Waziri Ummy amezita Hospitali za Wilaya na Mikoa watenge pesa kwaajili ya kuwasomesha madaktari wao kwani Rais Samia ameonesha kwa vitendo kutoa pesa hiyo kwa mabingwa na wabobezi.

 

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI