UKUSANYAJI WA MAPATO KWA NJI ISIYO YA KODI UMEONGEZEKA ZAIDI YA BILIONI 852


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOOMA

OFISI ya msajili mkuu wa serikali imesema ukusanyaji wa mapato kwa njia isiyo ya kodi umeongezeka kwa kukusanya kiasi Cha shilingi bilioni 852.98 sawa na asilimia 109.5 kwa   juni 30 2022  na Lengo ilikuwa kukusanya shilingi bilioni 779.03 na asilimia 33.5 zaidi ya kiasi kilichokusanywa juni 2021 ambacho kilikuwa bilioni 638.87.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa uwekezaji wa umma kutoka ofisi ya msajili wa  Hazina, 
Lightness Mauki wakati akizungumza na wanahabari oktoba 26 Jijini Dodoma  kuhusu mafanikio ya ofisi hiyo amesema ufanisi huo umechangiwa na kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya uwekezaji wa mitaji ya Umma.

Pia amesema ni  Pamoja na hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali katika kukuza mapato na kudhibiti matumizi  na kuongezeka kwa shughuli za ufuatiliaji katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa chache .

Aidha amesema Ofisi inaendelea kusimamia utendaji katika Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache ambapo, pamoja na mambo mengine, Serikali imefanikiwa kufanya majadiliano na Wanahisa wenza kwa lengo la kuboresha utendaji wa  Kampuni hizo ili kuhakikisha Serikali inapata gawio pamoja na kuongeza idadi za hisa. 

 Hata hivyo  Mkurugenzi hiyo ameongeza kuwaOfisi ya Msajili wa Hazina kama msimamizi mkuu wa uwekezaji wa Serikali kwa niaba ya Mheshimiwa Rais itaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa Taasisi na Mashirika yaUmma ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata marejesho ya uwekezaji wake sambamba na kuongezeka kwa mapato yasiyo ya kodi ili kusaidia miradi ya maendeleo kwa faida ya Taifa na wananchi wote kwa ujumla. 

Ofisi ya Msajili wa Hazina  imeanzishwa kupitia Sheria ya Msajili wa Hazina  Sura 370. Kwa Lengo kuu la kusimamia uwekezaji na mali zingine za Serikali katika taasisi na mashirika ya umma, pamoja na kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa hisa au kuna maslahi ya umma kwa niaba ya Rais na kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. 


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI