KAMPENI YA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO WALIOCHINI YA MIAKA 5 KUANZA KESHO NCHI NZIMA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WATANZANIA wametakiwa kutoa kutoa ushirikiano  Kwa watoa huduma wa Chanjo ya Polio pindi wanapowaona Kwa kuwatoa watoto wao walio chini ya umri wa miaka mitano  ili wapate Chanjo ya Polio ya matone kwa lengo la kuongeza kinga dhiki ya ugonjwa wa Polia ambao ni mkali na una madhara makubwa  wa watoto hao.

Hayo yamesema leo Novemba 30,2022 jijini hapa na Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma  Dk. Francis Bujiku  wakati akifunga mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyolenga uhamasishaji wa Chanjo hiyo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), amesema ugonjwa wa Polio una madhara makubwa kwa watoto hao.

Pia amewashukuru waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuharakisha jamii inapata uelewa wa masuala ya chanjo.

Naye mwzeshaji wa mafunzo hayo Afisa Program ya Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Lotalis Gadau amesema kampeni hiyo inaanza 1 hadi 4 Disemba mwaka  huu katika mikoa yote nchini .

Amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwafikia watoto zaidi ya milioni 14 katika awamu ya nne ya utoaji wa chanjo hiyo na kwamba kutakuwa na wasimamizi wa kitaifa ambayo watasaidia mikoa yote  katika kampeni hiyo.

Afisa huyo ameeleza zoezi la chanjo litafanyika nyumba kwa nyumba na kisha nyumba ambayo itakuwa imepata chanjo itawekwa alama ya tiki ili kuonesha tayari imekwisha kupata huduma lengo likiwa ni kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo na kuepusha usumbufu wa foleni na upotevu wa muda.

"Matarajio yetu kwa waandishi wa habari ni kutoa Kipaumbele kuandika habari za chanjo za watoto,kuwa na agenda ya  kudumu ya habari za afya za watoto pamoja na kuwahimiza wanahabari kuelimisha katika afya za kila siku za afya zitolewazo na sekta ya afya," amesema.

Pia ametaja njia za maambukizi ya ugonjwa huo  na dalili ikiwa ni pamoja na homa, uchovu, maumivu, ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya Viungo.

Ameongeza kuwa ugonjwa huo huambukizwa kwa kuingia mwilini kwa njia ya mdomo, kunywa Maji,au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa Mtu aliyeambukizwa virusi hivyo  virusi huongezeka ndani ya utumbo na hutolewa na mtu aliyeambukizwa kwenye kinyesi, ambacho kinaweza kupitisha virusi kwa wengine.

Post a Comment

0 Comments

ENDELEENI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI” MHE. NDERIANANGA