VETA RUVUMA YABUNI KIFAA CHA KUFUNDISHIA UMEME WA MAGARI


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

VIJANA wametakiwa kujibweteka na kutokukaa nyumbani bila kazi ya kufanya Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), kupitia Vyuo vyake inapokea wanafunzi wanaojua kusoma na kuandika na wale waliomaliza Vyuo vikuu kwenda kujifunza elimu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam juzi katika banda la Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"
Mwalimu wa Somo la   Umeme wa magari (Auto Electric),kutoka  Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), Mkoa wa Ruvuma wilayani Songea Andrea Shayo amesema mwanafunzi aliyehitumu fani ya ufundi wa magari hawezi kulala njaa Kila siku kwani  zonaongezeka na zinahitaji kufanyiwa huduma ya utengenezajihivyo muda na sehemu yoyote anaweza akapata ofisi na kwamba sio lazima awe na sehemu ya nyumba akiwa anaelewa ufundi vizuri muda wowote atapigiwa simu na kwenda kutatua matatizo

Shayo akizungumzia kifaa  kinachujulikana  kwa jina la 'Auto Electric, Training Model' ameeleza kuwa kifaa hicho  ni kifaa cha kufundishia wanafunzi wanaosoma fani  ya umeme wa magari kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tatu na  umuhimu wake ni mwanafunzi huyo atajifunza kwa vitendo na nadharia na kumfanya apate uelewa zaidi.

Ameongeza kuwa kupitia kifaa hicho kazi ya kufundisha itakuwa ni rahisi kwa Mwalimu wa somo hilo na mwanafunzi kuelewa zaidi na kwa haraka.

Shayo ameeleza kuwa kifaa hicho kinamwezesha mwanafunzi kutengeneza vitu vya umeme kwenye gari kupitia teknolojia huku akitolea mfano gari inapokuwa haijafungwa mlango na watu waliopo ndani kama hawajafunga mikanda likiwashwa haliwezi kuwaka na kwamba kinalinda usalama zaidi.

Ameongeza kuwa katika kifaa hicho wameweka mfumo wa kielektroni ambapo giza likiingia gari itajiwasha taa yenyewe  huku akisema lengo la mfumo huo ni mwanafunzi apate kujua vifaa vya umeme vinafanyaje kazi.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA