Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Taaluma,Tafiti na Ushauri Elekezi Profesa Provident Dimoso ( Katikati), akifanya kipindi na moja ya kituo cha redio nchini alipotembelea banda la Chuo Cha Mipango lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dk. Jim Yonazi, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).
Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
TAKWIMU zinaonesha umasikini mwingi upo vijijini na moja ya utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP),
ilionekana moja ya sababu inayochangia umasikini wa wananchi ni kutegemea shughuli ya kilimo kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko nyingine.
Pia Chuo hicho kinawakaribisha wanafunzi kujiunga kwani ufundishaji wake ni wa vitendo na nadharia na kinatambulika na Serikali na baada ya kumaliza masoma mwanafunzi ana nafasi kubwa ya kuajiriwa na kujiajiri mwenyewe.
Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 05, 2023 Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Taaluma,Tafiti na Ushauri Elekezi Profesa Provident Dimoso alipotembelea banda la Chuo Cha Mipango lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema wanafunzi wa Chuo hicho wanatambuliwa na serikali.
"Chuo hiki ni cha serikali ambacho kipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, kimesajiliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), na pia kinatambuliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU), pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),na hii imekuwa ni kitu chema kwa wanafunzi wetu kupata mikopo,"amesema Prof. Dimoso.
Prof. Dimoso amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mkopo hiyo ambapo kwa sasa wanafunzi wa Chuo hicho wanasoma vizuri.
Makamu huyo amesema chuo cha Mipango kimeanzishwa mwaka 1979 na kupewa majukumu makubwa matatu, kutoa Taaluma, kufanya Utafiti, kutoa ushauri Elekezia huku akifafanua kuwa kwa upande wa taalum kimejikita kutoa kozi za muda mrefu na mfupi.
Ameongeza kuwa chuo hicho kinatoa
kozi za muda mrefu na mfupi huku akifafanua kwamba kozi zake ni pamoja na Astashahada (certificate),kwa mwaka mmoja, kozi ya diploma mika miwili, degree miaka mitatu na kozi ya Masters degree miaka miwili pamoja na Post graduate diploma mwaka mmoja.
Prof.Dimoso ameeleza kuwa kozi zote hizo zinatambuliwa na serikali
wanafunzi wanapomaliza kozi hizo wanapata umahiri wa kutosha wa kuajiriwa na serikali au mashirika mbalimbali ya kimataifa.
"Chuo hiki kina jukumu la kufanya tafiti mbalimbali na moja ya tafiti tulizofanya hivi karibuni ni tafiti ambayo inahusiana na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na umasikini," amesema.
Ameongeza kuwa tafiti hiyo imeonekana wananchi wengi vijijini na zaidi ya asilimia 65 ya watanzania wanaishi vijijini hivyo chuo hicho kinahudumia watanzania wengi zaidi
0 Comments