TCAA YASOMESHA MARUBANI WAZAWA ILI KUPUNGUZA GHARAMA

Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam 

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA), inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa marubani hali inayosababisha rubani kufanya kazi zaidi ya kampuni moja hiyo mamala  imeanza kuwasomesha marubani hao kupitia Mfuko wa Mafunzo lengo ni kukidhi Soko la ndani katika sekta ya Anga.

Pia Mamlaka hiyo  imevifungia viwanja vya ndege 300 vilivyopo kwenye mapori
kwa kutokuwa na vigezo vya kurukia ndege kutokana na mamalaka iliyonayo ya kusimamia ujenzi wa viwanja hivyo pamoja na huduma za ardhini.

Akizungumza Julai 5 kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),
Hamza Johari amesema lengo la kuwasomesha marubani hao ni kupunguza uhaba uliopo wa marubani hasa wazawa.

Johari amesema wanafuanzi  kutokupenda somo la hesabu ndio chanzo cha upungufu wa marubani hivyo wameanzisha klabu za wanafunzi ili kuwajengea uwezo huku akiwashauri wanafuanzi walipende somo hilo litakalowapa nafaisi ya kusomea fani ya urubani.

Mkurugenzi huyo amesema mbali ya changamoto hiyo  sekta ya Anga inakabiliwa na uhaba wa miundombinu.

Ameongeza kuwa (TCAA) wanatoa leseni kwa ndenge nyuki(droni)ambapo mtoa huduma hiyo anapaswa kuwa amesajiliwa na kupatiwa leseni.

Mamlaka ya usafiri wa anga TCAA mpaka Sasa wanasimamia anga lote la Tanzania na Rwanda.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU