PURA: MRADI WA LNG KUGHARIMU TIRILIONI 97, AJIRA ZAIDI YA 10,000 ZITAPATIKANA KWA WATANZANIA

Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam 

MRADI wa kuchakata na kusindika gesi Asilia (LNG) utagharimu kiasi cha Dola za Marekani bilioni 42 sawa na fedha za kitanzania  trilioni 97 ambapo kuweka Mtambo nchi kavu Dola bilioni 7 wakati wa ujenzi na kwamba fedha hizo zitaingia kwenye mfumo wa uchumi wa Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 5,2022, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni alipotembelea banda la mamala hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema mradi huo ni mkubwa.

Mkurugenzi huyo akizungumzia suala la ajira wakati wa ujenzi wa mradi huo ameeleza kuwa  utaajiri Watanzania hadi 10,000 na   baada ya ujenzi wakati wa oparesheni wanatarajia utaajiri na wengine kati ya 400 hadi 600.

Amesema sekta nyingine zitafaidika kwa namna moja au  ikiwamo ya kilimo, malazi, usafirishaji na kwamba 
Serikali imeshapanga eneo linalozunguka Mtambo litakuwa ni maalumu kwa uchumi na litatengwa kwa ajili ya viwanda ambavyo vitatumia gesi ambayo itabaki nchini.

"Gesi ambayo itatumika nchini tunatengemea kuanza kutumika eneo la karibu na kiwanda cha kuchakata na kwa sasa tupo katika hatua mbalimbali za kukamilisha mazungumzo katika mradi huu kuna vitalu ambavyo viligundulika vya gesi zipo bahari kuu ambayo ina kina kirefu kutoka ardhini yenye kimomita 160 kutoka ufukweni," amesema Mhandisi Sangweni.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa gesi hiyo iligundulika kutoka katika vitalu namba moja, mbili na namba nne na kwamba kitalu namba tatu gesi iliyokundulika ilionekana haiwezi kuwekezeka kutokana na gharama za uwekezaji wake ni kubwa kuliko gesi iliyopo.


Amefafanua kuwa gesi iliyokundulika katika kitalu namba moja, mbili na nne serikali ilikaa na wawekezaji na kuamua ili ibadilishwe kuwa fedha kwa haraka na ililenga kupeleka masoko ya mbali.

"Ili uweze kupeleka gesi kwa wingi lazima uibadili ili iwe kwenye mfumo wa maji maji ili uibebe nyingi, kwa Tanzania tumewaka mabomba kwa sababu umbali wa kuitoa gesi na kuileta kwenye matumizi ni ndogo lakini iwapo gesi hii tutaipekelaka zaidi ya kilomita 250 basi inabidi uangalie ni namna gani ya kutumia zaidi ya kutumia bomba," Ameongeza.
 
Tumeamua kuweka mradi wa kuibadili gesi hiyo kwa kuipooza kuwa kwenye hali ya maji na kwamba ili gesi ipoe na kuwa katika hali hiyo inabidi ipoozwe chini ya nyuzi 'Negative'162 na ni Mtambo maalumu ambao hutengenezwa, unawekwa ambapo inapitishwa gesi hiyo na kubalika kwa kuwa katika hali ya maji," amesema.

Amesema Mtambo huo umewekwa nchi kavu katika eneo la Lindi ndipo utakapo jengwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo awali mazungumzo yalifanyika na yapo katika hatua za maamuzi ya timu ya serikali, wataalam na timu ya wataalam kutoka katika kampuni ambayo yalifanyikia jijini Arusha tangu Novemba 8, mwaka 2021 na kumalizika Mei 19, mwaka 2023.

"Mimi ndio nilikuwa mwenyekiti wa timu ya serikali na mazungumzo haya yalihusisha makubaliano ya mikataba mitano," amesema.


Akizungumzia mikataba hiyo amesema mkataba wa kwanza ni wa nchi hodhi ambao umeainisha misingi ya uwekezaji ugawanaji na utekelezaji wa mradi wenyewe kwa kuzingatia kila upande 
Serikali, wawekezaji ikiwamo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Amesema mkataba wa pili ni wa ugawanaji mapato unaoendana na mradi ambapo waliuboresha na kwamba walijadiliana juu ya mkataba wa ukodeshaji ardhi ambayo utajengwa Mtambo huo ambapo utamilikiwa na TPDC hivyo lazima waingie mkataba na kampeni ambazo zitawekeza.

Amebainisha kuwa gesi hiyo itashafirishwa kwenda nchi za mbali kupitia meli maalum ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba LNG na kwamba mkataba wa nne walioingia ni kuangalia namna gani wa kuitumia Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA).

Ameeleza kuwa mwisho walifanya makubaliano ya  ulinzi wa miundombinu ambayo itajengwa na kwamba wao kama serikali walisema wazi jukumu hilo la miradi ya kimkakati nchini ni la Jeshi la wananchi.

Amesema mkataba, makubaliano yakikubalika yatasainiwa TPDF pamoja na kampuni huku akisema mikataba hiyo mitano waliisimamia katika kujadiliana na walihusishwa wataalam kutoka kwenye maeneo mbalimbali wakiwamo TPDF, TPDC na TPA wote ambao waamini mradi huo utaenda kuwanufaisha.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU