TTCL KUZIUNGANISHA KIDIGITALI NCHI AMBAZO HAZINA NAFASI YA KUIFIKIA BAHARI YA HINDI

Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL),linatarajia kuziunganisha nchi ambazo hazina nafasi ya kufikia Bahari ya Hindi ambapo zitaunganishwa kupitia digitali lengo likiwa ni kuongeza Pato la Taifa kupitia fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam Julai 03,2023 na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Zuhura Muro wakati alipotembelea banda la TTCL katika 
Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo "Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema Tanzania itaongeza Pato la fedha za kigeni kwa kuuza Ubunifu, Teknolojia nje ya nchi kupitia shirika la TTCL.

Muro amesema shirika hilo linauwezo wa kuifanya Tanzania ikawa ni nchi kiongozi sio tu kiteknolojia bali kiuchumi ,kiusalama katika ukanda na kiutamaduni.

"Tukiweza kukuza huduma za kidigitali tutakuza utamaduni wa Tanzania nje ya nchi kupitia digitali kwenye runinga na redio zetu na huduma nyingne za mawasiliano, nimefurahia sana maendeleo yanayopatikana katika shirika hili kwa kuwa linaweza kuwa muhimili mkubwa katika kuhifadhi data za wafanyabiashara," ameongeza.

"Nimepata fursa ya kutembelea banda letu Leo na nimefurahi kutokana na unyeti  wa shirika hili kwa Taifa letu hasa tunapozungumzia uchumi wa kidigitali, tunaamini Shirika hili likifanya vizuri katika mawanda ya kidigitali uchumi wa tanzania utapaa kwa sababu  dunia ya sasa ni ya kidigitali na shirika linawezesha hali hii ya mafanikio kama mlivyoona "amesema Muro.
 
Amesema TTCL imefika mahali inatangza Utalii wa Tanzania kwa kiwango kikubwa huku akisema nguvu walioyoiweka katika mkongo wa Mawasiliano wa Taifa unaunganisha nchi kila kona hivyo gharama nyingi za mawasiliano zitapungua.

Mwenyekiti huyo amesema TTCL itapunguza gharama hizo nchi itakuwa na maingiliano yenye tija zaidi na kuwezesha uchumi wa Taifa kwenda mbele na kwamba shirika hilo halitaishia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na kati katika nchi za (SADC).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Peter Ulanga, amesema Shirika hilo linabeba uchumi wa Tanzania wa kidigiti kama nguzo muhimu ya uchumi huo hapa nchini na kwamba wanashirikiana na serikali bega kwa bega kuhakikisha uchumi unakua na kwenda katika maeneo makubwa ya kimaendeleo nchini.

Ameongeza kuwa wamekabidhiwa na nchi kuendesha mkongo  wa Mawasiliano wa Taifa na kwamba kwa sasa wanapatikana  katika nchi Saba ambapo wanatarajia kuunganisha nchi  ya nane ambayo ni Congo Mashariki.

"Kipekee kabisa napenda kuwakaribisha wananchi katika banda letu,tunatoa huduma mbalimbali kwa ukubwa sisi ndio tumekabidhiwa na nchi kuendesha mkongo wetu wa mawasiliano wa Taifa," ameeleza Ulanga.

Ameongeza kuwa wao kama TTCL wanajaribu kubadilisha mtazamo wa matumizi ya Intaneti  badala ya kuwa na vifurushi wanatoa Intaneti bila kikomo kwa njia ya huduma ya 'Fiba mlangoni kwako'.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI