UDOM YAJA NA MFUMO WA KUDHIBITI HALI YA HEWE KILIMO CHA 'GREEN HOUSE'


Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam

CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM),kimebuni teknolojia ambayo itawasaidia wananchi hasa waliojiingiza katika kilimo cha  kitanda nyumba (Green House) katika kutambua kulima  aina gani ya zao kutokana na hali hewa iliyopo katika eneo husika ambacho ni 'Greenhouse control system'.

Mfumo huo unaodhibiti hali ya hewa, ikiwemo unyevunyevu na joto, kwenye kilimo cha kwenye 'greenhouse' na kumrahisishia mkulima kubaini mkulima alime zao gani analolitaka, kulingana na mazingira ya eneo ama mkoa husika.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana ,Mwanataaluma kutoka Idara ya Fizikia, Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati, UDOM,Paschal Magambo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), maarufu SabaSaba, amesema  ubunifu huo umefanyiwa majaribio na kubaini unaweza kujibadilisha kulingana na mazingira ya sehemu mbalimbali kwa kutumia kifaa maalumu kitakachofungwa kwenye 'greenhouse'.

Magambo ameeleza kuwa tofauti ya green house zilizopo sokoni ni zimetengenezwa kudhibiti wadudu pekee na kwamba  kilimo hicho ni tofauti na Kilimo kingine kwa mfumo huo unauwezo wa kudhibiti hali ya hewa kulingana na eneo husika.

Ameongeza kuwa mfumo huo unaweza kuchagua aina ya zao, mfano tikiti au nyanya na itakuonyesha ni joto la aina gani linahitajika, ili zao likue.

Naye Mkufunzi kutoka chuo hicho, Dk. Mhandisi, Ombeni Mdee, amesema Chuo hicho UDOM linaendelea na ubunifu katika maeneo tofauti ikiwamo kubuni pampu ya maji inayotumia umeme mdogo, ili kupunguza matumizi ya nishati.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI