Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam
WAZAZI, wananchi wametakiwa kufika katika banda la Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),katika
Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo "Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," lengo likiwa ni kujua fursa zinazopatika ili kuwapatia vijana nafasi ya kusomea ujuzi wanaohitaji.
Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 03,2023 katika maonesho hayo Mwalimu wa Bidhaa za Ngozi kutoka chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),Dakawa mkoani Morogoro
Hamidu Mahembe amesema ada ni nafuu ambazo mtu yoyote anaweza kuzimudu kulipa ambapo kwa kipindi cha miaka miwili mwanafunzi wakutwa analipata ya hiyo ya shilingi 60,000 na kukaa bwenini analipata 120,000
Mahembe amesema serikali ndiyo inawasomesha vijana hao kupitia Vyuo vya VETA kwa wale wanafunzi wa muda mrefu.
Amesema kuwa bidhaa za ngozi zimegawanyika katika sehemu mbalimbali zikiwamo viatu, mikoba na mikanda.
Ameongeza kuwa katika Chuo hicho wanatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kulingana na mteja wao na kwamba kijana akimaliza mafunzo hayo anakuwa na umahiri wa kutengeneza bidhaa hizo za ngozi.
"Wapo vijana wetu waliomaliza Chuo Cha VETA Dakawa wameajiriwa katika viwanda mbalimbali na vikubwa vinavyojulikana kwa uzalishaji wa bidhaa zenye ubora," amesema.
Ameeleza kuwa ujuzi unamkomboa mwanadamu na VETA ipo kwa ajili ya Watanzania ili kupata ujuzi huo wa kuweza kuajiriwa au wa kujiajiri lengo likiwa ni kukuza kipato katika jamii na kwa nchi.
0 Comments