Na Asha Mwakyonde Dar es salaam
MAMLAKA ya Masoko ya Mtaji na Dhamana (CMSA),inaendesha kozi fupi kila mwaka lengo likiwa ni kuongeza ujuzi kwa watendaji wa masoko na kwamba kozi hiyo imeshafanyika zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 03,2022 Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma kutoka katika mamlaka hiyo
Stella Anastazi katika banda la CMSA lililopo jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kuanzisha masoko mawili ya mitaji ambayo ni Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE),ambalo lilianzishwa mwaka 1998 na soko la Bidhaa Tanzania lililoanzoshwa mwaka 2016.
Stella ameeleza kuwa Pamoja na masoko hayo mamlaka pia inatoa leseni kwa watendaji mbalimbali wa masoko mfano leseni ya Meneja Mfuko, leseni ya mshauri mwekezaji na leseni ya mtunza amana kwa ujumla na kuna leseni sita ambazo zinatolewa na mamlaka.
Amesema kwa mtu yoyote anayetamani kuwa mtendaji wa masoko ya mitaji katika eneo lolote akifika katika banda hilo atasikilizwa pamoja na kupatiwa ushauri kulingana na mpango wake wa kuomba leseni ya aina gani.
"Mamlaka katika jitihada za kuhakikisha mtendaji wa soko anafanya kazi kwa weledi katika viwango vya kimataifa vinavyoleta tija kwa sekta ya masoko ya mitaji na nchi kwa ujumla," amesema na kuongeza.
"Tunawakaribisha wananchi wale ambao wanatamani kujua kuhusu masoko ya mitaji na fursa zake," ameeleza Stella.
Taasisi yetu ni ya serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya mitaji ya mwaka 1994 kifungu namba 79 ambapo sheria hiyo imetoa majukumu mbalimbali yakiwamo kuanzisha, kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji, kumlinda mwekezaji anayewekeza kwenye soko hilo pia kuishauri serikali katika masuala yanayohusu uwekezaji wa masoko ya mitaji.
0 Comments