MOI YAJA NA SULUHISHO LA WENYE MAUMIVU YA MGONGO

Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

TAASIASI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),imeanzisha matibabu, kiliniki maalumu kwa kutumia teknolojia ya kisaaa kwa wagonjwa wenye shida ya maumivu ya mgongo kwa muda mrefu ambao wamepatiwa matibabu sehemu mbalimbali kwa kupatiwa vidonge vya maumivu.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 03,2022  katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo "Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"
Daktari  wa mifupa kutoka MOI, Dk.Sharifu Luena amesema kuwa watu wenye shida hiyo wafike katika taasisi hiyo kufanyiwa vipimo na kupata matibabu hayo maalumu kwa ajili ya kumaliza tatizo la muda mrefu.

"Ninafuraha ya kuwakaribisha Watanzania wote katika banda letu hapa Saba Saba ambalo linapatikana katika banda la Jakaya Kikwete tumeandaa vitu vingi vya kuonesha katika msimu huu wa Saba Saba pia kuwaonesha Watanzania jidihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi," amesema.MOI 

Dk. Luena ameongeza kuwa taasisi hiyo bado inaendelea kutoa huduma za kibingwa zinazohusisha kubadilisha nyonga, kufanyiwa upasuajia wa kisasa wa mgongo na kichwa.

Aidha amewaomba wenye matatizo ya migogoro, kichwa, miguu kufika katika banda hilo ili waweze kunaonana na madaktari bingwa kwa matibabu ya kibingwa zaidi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI