DODOOMA KUFUNGA MWAKA 2022 KWA KUPANDA MITI


 Na Asha Mwakyonde, Dodooma

MKUU wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wakazi wa Dodoma na wadau wengine kupanda miti aina ya Migunga katika bonde la Mzakwe na maeneo mengine yaliyopo mkoani humo kupanda miti.

Kampeni ya upandaji miti Mkoa wa Dodoma inayotarajiwa kuanza Disemba 31hadi msimu wa mvua utakapokwisha huku  ikilenga Halmashauri zote nane za Mkoa huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu  kampeni ya upandaji miti leo Disemba 30,2022,jijini Dodoma Senyamule ameeleza miti ndio aina pekee inayoweza kustahimili ukame.

Amesema lengo kuu la Mkoa WA Dodoma ni kila Halmashauri kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka licha ya baadhi ya maeneo kupewa kipaombele kama eneo la Ihumwa kwenye chanzo cha maji cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA), na katika bonde la Mzakwe.


Mkuu huyo wa mkoa wa amesema mkakati wa mkoa wa huo kwa kushirikiana na wadau wa mazingira umeanza kampeni ya kupanda miti, kampeni ambayo imeambatana na maagizo.

Aidha Senyamule amesema kuwa kutokana na wananchi wengi kutojiwekea utamaduni wa kupanda miti amewataka wananchi kupanda miti isiyozidi mitano katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa Senyamule ili kuhakikisha taifa linakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, sheria inaitaka kila halmashauri nchini kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Aidha  ameongeza kuwa Wakala wa misitu (TFS),wamezalisha miche ya miti ya kutosha katika kitalu cha miti eneo la Mailimbili na kwamba  miche hiyo  inagawiwa bure, huku akitoa  rai kwa wanadodoma kwenda  kuchukua miche ya miti na kupanda katika maeneo yao.

 "Tutapita kukagua kila nyumba na kuona miti mitano iliyopandwa na wale wasiopanda watachukuliwa hatua kwa kuwa hii ni sehemu yasheria ndogo tulizonazo kwenye Halmashauri” Ameongeza Senyamule.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI