BRELA YAMKABIDHI SWEDI LESENI YA BIASHARA KUNDI "A"


Afisa Usajili Mwandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Lugano Mwampeta (kushoto), akikabidhi Leseni ya Biashara Kundi "A" kwa mfanyabiashara Bw. Hassan Swedi katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji kwa mkoa wa Mbeya, yaliyoanza  tarehe 14 Machi, 2023 katika wilaya ya Chunya mkoani humo  na yatahitimishwa  tarehe18  Machi, 2023.  Katika maonesho hayo BRELA inatoa elimu, pamoja na huduma za papo kwa papo za Sajili na utoaji wa Leseni za Biashara kundi "A".

Maafisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakitoa elimu kuhusu urasimishaji wa biashara  kwa kundi la wachimbaji wadogo wa madini, katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji kwa mkoa wa Mbeya. Maonesho hayo yanafanyika  Wilaya ya Chunya na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 18  Machi, 2023. BRELA inashiriki maonesho haya kwa kutoa elimu, huduma za papo kwa papo za Sajili na Utoaji wa Leseni za Biashara Kundi "A"



Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA