TANTRADE NA UBALOZI WA MISRI KUAANDA MIKUTANO YA B2B KATIKA SEKTA YA HOTEL NA VIFAA VYA NYUMBANI


Dar es Salaam 

MKURUGENZI Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis  Juni 20, 2023 katika ofisi za TanTrade amekutana na Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Ukiongozwa na Ndugu Mohammad Ally Atteya na Bi. Leila Adel, ambapo wamezungumzia maandalizi ya Maonesho na Mikutano ya B2B katika sekta ya Hotel na Vifaa vya nyumbani  kutoka Misri.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Julai 17-19 , 2023, Zanzibar ambapo Kampuni takriban 15 za Misri kwenye Sekta ya Utalii zitashiriki.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema TanTrade itashirikiana na Ubalozi wa Misri katika uratibu kwa kutoa wataalam  kutoka TanTrade Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo.

Katika Mkutano  huo kutakuwa na Maonesho madogo ya Bidhaa pamoja na mikutano baina ya wafanyabiashara (B2B) wa Tanzania Misri.

Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha kutembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13,2023 katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU