CMSA: THAMANI YA UWEKEZAJI KWA MASOKO NA MITAJI YAFIKIA TRILIONI 35


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MAMLAKA ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), kwa kushirikiana na  Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),imewajengea uwezo wafanyabiashara kutoka Kanda ya Kati lengo likiwa ni kuwezesha kampuni ndogo na za kati.

Pia imeelezwa  kuwa Tanzania inafanya vizuri katika suala la Masoko na mitaji na kutokana na ufanisi huo inashika nafasi ya tano mbele ya Nchi za Afrika Kusini,Misri,Mouritius na Nigeria.

Hayo yameelezwa Juni 20,2023 na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana(CMSA) ,Nicodemas Mkama wakati akifungua semina ya siku moja  kwa wafanyabiashara yenye lengo la kuwawezesha wenye Kampuni ndogo na za kati ambapo hadi sasa 
thamani ya uwekezaji kwa masoko na mitaji imefikia Shilingi Trilioni 35.


"Leo tunasemina na wananchama wa SIDO wa Kanda ya kati ikijumuisha mikoa ya Dodom,  Manyara, Singida na Tabora, tunawajengea uwezo kuweza kutambua fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji hivyo wataweza kukuza Kampuni zao kuhakikisha biashara zao zinaendeshwa katika viwango ambavyo vitawasaidia kupata masoko na kukidhi matakwa ya masoko hapa nchini," ameeleza.

Ameongeza kuwa siku hiyo ni muhimu ya sekta ya fedha hapa nchini ambapo wanachama hao wataweza kutumia fursa ambayo imeendaliwa na CMSA kwa kushirikiana na SIDO.

Mkama amesema thamani hiyo inaonesha ni jinsi gani masoko hayo ni muhimu katika kuendeleza uchumi ambapo kampuni mbalimbali zinatumia masoko hayo kupata fedha.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wananchi kiuchumi,Bhoke Manyori amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya kupewa ushauri wa kifedha bila kuambiwa wafanye biashara zipi.

Naye Mfanyabiashara Komba Jumbe amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya uelewa kuhusu masoko na mitaji na kutoamini.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU