TGNP YADHAMIRIA KUHAMASISHA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa kushirikiana na  wadau wa maendeleo Aga Khan Foundation pamoja na Global Affairs Canada  wanatekeleza Mradi wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika mikoa mitatu ya Morogoro, Dodoma na Mtwara lengo likiwa ni kuandika habari zenye Mrengo wa kijinsia ambazo zinamsema vizuri mwanamke katika jamii.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma hivi karibuni na  Mratibu wa mafunzo hayo kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari zenye Mrengo wa kijinsia katika kuhamasisha wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya familia hadi za juu kwa kumuandika vizuri mwanamke kwa kutumia misemo hasi kuwa chanya.

Ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya vitongoji,mitaa, vijiji, madiwani hata katika nafasi za ubunge.


Mzurikwao amefafanua kuwa wanaamini  waandishi wa habari ni wadau wa maendeleo na kwamba taarifa wanazo ziandika kuhusu wanawake wanatamani ziwe na Mrengo wa kijinsia ambazo zinamsema vizuri mwanamke, kuhamasisha ili aweze kuchukua hatua ya kugombea nafasi mbali mbali zilipo kwenye jamii za kisiasa na hata nyingine.

"Tunatambua kuwa kwenye jamii yetu kuna misemo hasi inayohusiana na masuala ya wanawake pamoja na wanawake na uongozi, misemo hii nyie kama waandishi wa habari mnaijua, mnaongeleaje misemo hii ambayo inamuweke chini mwanamke na ikifika mahalia anakuwa hawezi kugombea nafasi ya uongozi, tunawezeje kuigeuzana kuwa chanya ihamasishe, imseme vizuri jamii iweze kujua kwamba hata mwanamke anaweza akawa kiongozi mzuri," amesema.

Ameongeza kuwa waandishi wa habari wapo katika nafasi nzuri ya kuhakikisha jamii inabadilika huku akisema kwamba wao kama TGNP kabla mwandishi hayaenda kuibadilisha jamii hiyo  wameona wawapatie mafunzo ili wawe na mtazamo chanja kuhusu wanawake na uongozi kwenye ngazi tofauti tofauti.


Mzurikwao amesema wanatekeleza Mardi wa kujenga uwezo kwa waandishi wa habari kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo ya jamii The Aga Khan Foundation pamoja na Global Affairs Canada ili kuweze kuwajengea uwezo waandishi hao kuripoti habari zenye Mrengo wa kijinsia na kuwahamasisha wanawake wengine zaidi waweze kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.


Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Dk.Ananilea Nkya ameeleza kuwa kuna kazi nyingi wamefanya viongozi wanaume na wanawake ambapo wanawake hao hawapo kwenye nafasi za uongozi.

"Wanawake hawa wameweza kuonesha uwezo katika uongozi lakini tumeweza kuandika? Na kama hatuandiki watu mtamchaguaje mwanamke kuingia kwenye uongozi?,"amehoji.

Pia amewaasa waandishi wa habari kuwa ni muhimu  habari iwe inajikita kwenye jambo moja tu  isichanganye mada nyingi tofauti tofauti huku akitolea mfano uongozi wa kiongozi fulani umewezesha wananchi kupata maji na zahabati.


Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo Mariam Matundu  kutoka radio Dodoma  na runinga ya Dodoma paa  na Saleh Lujuo wamesema kuwa mafunzo hayo yamewabadilisha kutoka katika mtazamo hasi kwenda chanya.

Matundu amesema kuwa katika mafunzo hayo kitu kikubwa na cha pekee alichojifunza ni namna ya kuweza kutumia misemo hasi ambayo ipo kwenye jamii inayomkandamiza mwanamke.

" Sikuwahi kujua kwamba unaweza kutumia misemo hasi na kuibadilisha kuwa misemo chanya ambayo inaweza kutumika kuibadilisha jamii hiyo hiyo ikaweza kuamini mwanamke anaweza masuala ya uongozi," ameeleza Matundu.

Naye mwandishi wa Habari Saleh  Lujuo amesema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia mafunzo hayo huku akisema wao kama wanahabari wamezoea kuandika habari za viongozi wakubwa, maarufu.

Amesema katika mafunzo hayo ameona ni namna gani mwandishi anatakiwa kubadilika kuandika habari ambazo zitakazo leta faida na wananchi wakafurahi kupata kitu ambacho wanakihitaji.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI