NAIBU SPIKA ZUNGU: WATANZANIA MSIMBEZE RAIS DKT. SAMIA

Dar es salaam 

NAIBU Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu,  amewataka wa Tanzania wasimbeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameleta maendeleo makubwa katika nchi hii.

Naibu Spika Zungu alisema hayo katika mkutano wa hadhara jimbo la segerea uliowashirikisha wananchi wa Kimanga,Tabata, Kisukuru na Liwiti wa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuelezea kwa wananchi kazi  zilizofanywa na Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo. 

"Naomba watanzania msibeze Rais wetu Dkt ,Samia Suluhu Hassan  katika Taifa la Tanzania kaonyesha usawa na amani amefanya mambo makubwa kuna watu walikimbia Bungeni Rais amewafuata na wamerudi wamelipwa haki zao  "alisema Zungu.

Amewataka watanzania kudumisha amani na  kujenga umoja na mshikamano katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Wakati huo huo amemwagiza mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchukua hatua za haraka kufatilia mgambo wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam waache vitendo vya uonevu kwa wafanyabiashara wa mama lishe na Baba Lishe kuwamwagia biashara zao kila siku kwani ni vitendo vya uonevu.

Naibu Spika Zungu alisema endapo Mgambo wa jiji hilo wakiendelea kunyanyasa wafanyabishara hao na kumwaga vyakula vyao yatafika mbali  zaidi.

"Jamii yetu ni watu masikini sana  watu wanangaika na Biashara zao Mgambo wa Halmashauri ya jiji wanawaonea wafanyabiashara wa mama lishe na Baba lishe wanamwaga vyakula ni zambi kubwa sana wanarudi nyumbani bila pesa familia zao zinalala na njaaa "alisema Zungu

Akizungumza mkutano wa jimbo la segerea amempongeza Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kushirikiana na madiwani wake katika kutekeleza ilani na kuleta maendeleo kwa wananchi na kusimamia miradi ya maendeleo katika juhudi za kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan. 

Akizungumza katika  mkutano wa hadhara wa Jimbo la Segerea Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka mgambo kufuata taratibu za utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.

Mkuu wa Wilaya Eward Mpogolo alisema baadhi ya Mgambo tayari wamesimamishwa kazi kutokana na kukiuka taratibu za kazi yao .

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU