WALIOHITIMU CHUO KIKUU HURIA WAKUTANA, SERIKALI KUKIBORESHA


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma George Simbachawene amesema serikali itaendelea kuhakikisha inatatua changamoto mbalimbali za Vyuo vikuu nchini ikiwemo Chuo Kikuu huria lengo likiwa ni  kufikia Uchumi wa kati.

Hayo yameelezwa leo Septemba 21, 2023 Jijini Dodoma na Waziri  Simbachawene wakati akizungumza na Uongozi wa Chuo hicho katika Mkutano ulioshirikisha Jumuiya ya waliosoma katika Chuo Kikuu huria na kutaka kuja na mbinu mpya za ufundishaji kwa wanavyuo namna ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Amesema Chuo  hicho ni mkombozi kwa watu ambao wamekosa fursa ya kupata elimu ya juu kutokana na  changamoto mbalimbali.


"Hata mimi nilisoma hapa   nilikuwa nafanya shughuli zangu na najiendeleza kielimu kupitia hivyo inatupasa sisi kama jumuiya tushirikiane katika masuala ya kikiboresha ikiwamo miundombinu," amesema Simbachawene.

Kwa upande wake Mwenyekiti jumuiya ya chama cha wahitimu wa chuo hicho ambaye ni mbunge wa Tabora kaskazini Uyui Almas Maige ameisistiza Jumuiya hiyo kudumisha Umoja huo katika kukitangaza Chuo hicho ndani na nje ya Nchi.

Maige ameeleza kuwa ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kunakuwa na namna bora ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika na chuo kikuu huria kwani wengi ni wafanyakazi ambao tayari wapo kwenye ajira.

"Mkutano huu ni muendelezo wa majadiliano yaliyo bora hivyo chuo kinapata namna bora ya kihakikisha kila mwanachama anachangia ili kiwe kifedha, miundombinu yenye hadhi lengo likiwa ni kuhakikisha kinawafikia watu wote ndani na nje ya nchi na kukidhi soko la ajira," amesema Maige.


Naye Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima ambaye pia alihitimu katika Chuo hicho amekishauri Chuo Kikuu huria kuwekeza nguvu nyingi katika kufanya tafiti ili kuweza kutatua matatizo yaliyopo kwenye Jamii.

Ameongeza kuwa hawaoni matokeo ya tafiti zinazofanywa na wataaalamu huku  akiwashauri watafiti hao kushirikisha wananchi,
kuwahamasisha wanafunzi kujitegemea ili waweze  kujiajiri.

Makamu Mkuu kuu wa Chuo, Profesa Elifas Bisanda, ameeleza kuwa wanawahitaji wahitimu hao katika kukisaidia chuo yakiwamo masuala ya  harambee ili kuchagiza maendeleo ya miradi.

Ameongeza  tangu chuo hicho kimeanza kuhitimisha mwaka 1999 na kwamba  hawajawahi kuwatumia wahitimu wao licha ya kuwa ni  wadau muhimu  kwa maendeleo ya chuo  katika Nyanja mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI