Na Asha Mwakyonde Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA),imesema wadau wamekuwa na wasiwasi kuwekeza katika biashara ya ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari (CNG), ambapo Mamlaka hiyo inaendelea kuhamasisha wananchi kuwekeza kwenye eneo la matumizi ya Gesi hiyo.
Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo wakati Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko alipotembelea kwenye banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Nishati Bungeni jijini hapa ameeleza hali hiyo inatokana na upya wa biashara ya Gesi Asilia.
Amesema EWURA wamekuwa wakihamasisha ambapo hadi sasa kuna kampuni 20 zimeshonesha nia ya kuwekeza, katika ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi Asilia huku akisema wawekezaji hao bado wanajiuliza endapo biashara inalipa.
"Kutokana na hamasa ambayo tumeendelea kuitoa kwa wadau hali ya kurekebisha magari imeanza kufanyika wa kasi tofauti na awali," ameeleza Kaguo.
Kaguo amefafanua kuwa hadi kufikia mwaka jana magari yaliyokuwa yamerekebishwa yalikuwa 3000 kwa sasa ni yamefika, 4500 ambayo yamesharekebishwa hivyo kasi ya kurekebisha imekuwa kubwa .
Afisa huyo amesema kampuni zinazorekebisha magari kwa sasa zimeongezeka zimefika 10, na kwamba wandelea kuhamasisha zaidi.
0 Comments