JAMII YASHAURIWA KUWA NA UTARATIBU WA KUFANYA MAZOEZI, KUIPUNGUZIA SERIKALI GHARAMA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

SPIKA wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dk. Tulia Ackson amesisitiza jamii kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza lengo likiwa ni kuipunguzia mzigo serikali wa magonjwa yasiyoambukiza.

Pia amesema watu wote walioshiriki kuchangia mbio za Bunge Marathon kwa kutambua mchango wao kila mmoja jina lake litaandikwa kwa wino wa dhahabu na kihifadhiwa katika shule ya Bunge sekondari ya wavulana inayotarajiwa kujengwa ambapo siku yoyote mtu akitembelea pale ataona jina lake.

Hayo ameyasema jijini hapa leo,Aprili 13,2024, katika uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza baada ya mbio za Bunge Marathon zilizofanyika kwa lengo lakukusanya fedha kwa ajili ya kujenga Shule ya Sekondari ya Wavulana amesema Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kupambana na magonjwa hayo,hivyo jamii inapaswa kuthamini michezo.

Dk. Tulia aliongeza kuwa amefurahishwa mzee wa Miaka 91 kukimbia mbio za kilomita 10 na watoto kuanzia umri wa miaka 5 hadi 11 kukimbia mbio za kilomita 5 .

"Nimemuona pia mtu mwenye uhitaji maalumu amekimbia kwa kiti naye tutampa zawadi, nawashukuru kwa kujitoa kwenu ameeleza Dk. Tulia.

Spika Dk. Tulia ameeleza kuwa kulikuwa na mbio kuanzia kilimita 21, 10 na kilomita 5 na kwamba washindi wamepatiwa zawadi zao .

Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameongoza mbio hizo pamoja na wadau mbalimbali wa michezo na wengine kama Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya, Wabunge na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU