WAZAZI WATAKIWA KUWAHAMASISHA BINTI ZAO CHANJO YA HPV


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

ASILIMIA 70 ya wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi wanaofika katika vituo vya kutolea huduma ya afya hufika kwa kuchelewa na asilimia 21 hupoteza maisha.

Akizungumza jijini hapa Aprili 12,2024 Afisa Mpango wa Taifa wa chanjo
 kutoka Wizara ya Afya Lotalis Gadau wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi (HPV) , kampeni ya kuelekea maadhimisho ya wiki ya chanjo ambayo itaanza Aprili 22 hadi 28 mwaka huu.

Afisa huyo ameeleza takwimu kutoka taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaonesha kwamba Saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa kwa assilimia 36 ya Saratani zote na asilimia 21 huchangia kwa vifo.

Gadau alisema kuwa Chanjo hiyo ni salama na ni dozi ya Mara moja na inatolewa tofauti na awali ambapo ilikuwa inatolewa kwa awamu mbili kwa watoto wakike kuanzia umri wa miaka9 hadi 14.

"Ni muhimu sasa kwa wazazi kuhakikisha wanawahamasiha Watoto wao kujitokeza kupata Chanjo hiyo ya HPV ili kuwalinda na maambukizi ya ugonjwa huo, " amesema Afisa huyo.


Akifunga mafunzo hayo ya siku moja kwa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Dk.Tumaini Haonga alisema serikali kupitia Wizara ya Afya wanaendelea na juhudi za kuhakikisha wanatoa chanjo hiyo ili kuwakinga watoto na wanawake kwa ujumla.

Dk.Haonga alieleza kutokana na ugonjwa huo kuwa na Kinga Serikali imeamua kuwa na Mpango wa kutoa Chanjo hiyo kwa Watoto na mabinti ili kupambana na Saratani hiyo

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Saratani hiyo barani Afrika ambapo inakadiriwa takribani wanawake zaidi ya milioni 10 wanapata Saratani ya mlango wa kizaz kila mwaka huku milioni 6 barani.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI