JUMUIYA YA WAZAZI KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI KUONESHA MAPATO


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Hapi amewataka watendaji wa Jumuiya hiyo kila Mkoa kuandaa haraka taarifa za uhai wa Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na vikao lengo likiwa ni kutaka kujua watumishi hao na uhapakazi wao.

Pia Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ameeleza kuwa wanataka kufuta mfumo wa malipo ya fedha taslimu na kuanza kutumia ule wa kieletroniki ili mapato yote yaonekane.

Haya aliyasema leo Aprili 8,2024 jijini Dodoma katika mapokezi yake amsema wanatakaa kupokea taarifa za mail zote za Jumuiya na hali zake zikiwamo mashamba, magari,viwanja na changamoto zake.

Katibu huyo ameeleza kuwa lengo ni kutakaa kujua watumishi na uhapakazi wao na kwamba taarifa hizo zianze kuandaliwa haraka ambapo baadae atahamia kwa makatibu wa Wilaya na Mkoa .

Amesema kila mmoja ataeleza uhai wa Jumuiya hiyo katika eneo lake huku akisema itajulikana mbivu na mbichi lengo ni kuondoa ufanyaji kazi wa mazoea.

"Tuna kazi kubwa mbele yetu watendaji mpo hapa tutakuwa na kikao cha makao makuu tutazungumza tuone yale yote yaliyopo kwenye Jumuiya tuna taka kujua uhai wa Jumuiya, mali zote na hali zake," amesema na kuongeza.

" Tukaijenge Jumuiya ya wazazi tukavutie vijana na wale wa boda boda tuna uchanguzi mwaka huu na mwakani CCM tuna ilani ambayo ndio mkataba na wananchi," ameeleza Hapi.

MAADILI

Akizungumzia maadil Katibu Mkuu huyo amesema kuna mmomonyoko wa maadili wanataka kuona Jumuiya hiyo ikisimamia maadili mema na kufahatilia watoto shuleni.

Katibu huyo amesema ni lazima wasimame imara kusimamia maadili, ulinzi na maelezi ya vijana shuleni ili haki itendeke kwa waliofanyiwa vitendo visivyo na maadili.

Amesema viongozi wa chama hicho wanaandaliwa na kupikwa hivyo wanaccm wasifitiane na kwamba Rais Dk Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya uwekezaji kwenye miradi mikubwa ambayo inahitaji kusimamiwa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Zanzibar Ally Issa Ally ameahudi kumpatia ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja Katibu Mkuu huyo Hapi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Bara Joshua Mirumbe amesema wanajukumu la kupanga mikakati ili kuhakikisha chama hicho kinashinda uchanguzi za serikali za mitaa

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI