ALIYEHITIMU VETA AIOMBA SERIKALI KUMPATIA AJIRA KUSHONA SARE ZA JKT


Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MUHITIMU kutoka Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Songea,Riziki Ndumba, ambaye ni mtu mwenye ulemavu wa mkonoa meiomba serikali kuweza kumpa ajira kushona sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Ndumba amewataka vijana na watu wenye ulemavu wasijifiche nyumbani na badala yake wakasome ufundi katika vyuo vya VETA kwa lengo la kuwapunguzia kuwa tegemezi katika jamii zao huku akieleza vyuo hivyo vinafundisha fani mbalimbali.

Akizungumza leo Julai Mosi jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara (DITF), maarufu Sabasaba ameeleza kuwa kujiajiri mwenyewe anaweza huku akisema changamoto ya mtaji ni kikwazo cha kuwafikia malengo yake ya kiuchumi.

Kutokana na changamoto ya mtaji Ndumba anaiomba serikali kumpatia ajira katika taasisi zake zikiwamo Jeshi la Polisi na JKT ili aweze kujikwamua kiuchumi.

Ameeleze kuwa awali hakuwa na ujuzi wowote na kwamba baada ya kufika VETA na kusoma ufundi wa cherehani amekuwa fundi wa kushona nguo za aina yoyote.

 "Hakuna kitu ambacho kinashindikana mimi ni mtu mwenye ulemavu wa viungo VETA walinipokea na kunipatia ushirikiano ambapo kwa sasa nimekuwa fundi mzuri.

Aidha ameishukuru serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika shule za ufundi stadi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI