SELF KUWALINDA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA BIMA


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

MFUKO wa SELF umeanzisha huduma mpya ya bima kwa lengo la kulinda mali za wateja ili kuwawezesha waishi kwa amani hasa yanapotokea majanga mbalimbali. 

Pia mfuko huo una matawi 12 yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini ambako elimu ya fedha na bima inatolewa. 

Akizungumza Julai Mosi,2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, Afisa Bima katika Mfuko wa SELF, Rasuli Sadala, amesema huduma hiyo imeanzishwa kuwawezesha wateja waishi kwa amani hasa yanapotokea majanga mbalimbali.

Amesema kuwa kumekuwa na majanga mbalimbali yanatokea katika jamii ya watanzania ambapo ajili za moto,wizi hivyo kupitia bima hiyo itaweza kuwalinda wateja wake.

"Mfano ya wizi, moto, ajali mbalimbali na yanakuja bila mtu kuwa amejiandaa, lakini ukiwa na bima inaweza ikakulinda kulingana na majanga. Kwahiyo Mfuko wa Self umekuwa wakala kwa ajili ya kutoa huduma hizi kwa wateja wetu," amesema. 


Ameongeza kuwa edapo gari lako likipata ajali, kuungua moto au kuibiwa, kampuni ya bima itakufidia kukurudishia. Kuna bima za moto kwa ajili ya kulinda sehemu ya biashara, nyumba na bima za wizi ambazo zinalinda mali yako na bidhaa ambazo ziko kwenye maduka kwahiyo tunatakiwa tuishi kwa kujiamini,” amesema Sadala. 

Katika hatua nyingine alameeleza kuwa mfuko huo pia unatoa mikopo ya biashara na kilimo kwa taasisi na mtu mmoja mmoja yaani wafanyabiashara, wakulima, wafanyakazi kwa ajili ya kuboresha makazi. 

Amesema wanaendelea kuboresha mikopo ya vikundi ili kuwafikia wateja wa chini kwa lemngo la kuwainua Watanzania.

Sadala amewataka Watanzania kutembelea maonesho hayo katika banda la Wizara ya Fedha ambako wanapatikana ili kupata elimu ya fedha, huduma ya bima na mikopo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI