TSB YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI ZAO LA MKONGE, YA WEKA WAZI SIRI YA SOKO

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

WADAU wanaotaka kuwezekeza kwenye sekta ya Mkonge hawatakiwi kuhofia masoko ya kuuza zao la mkonge kwa kuwa moja ya jukumu la Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), ni kuwaunganisha wakulima na masoko ya mkonge.

Akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba), Afisa kilimo kutoka TSB, Emmanuel Lutego amesema kuwa Mkonge ni zao ambalo soko lake halitegemei msimu kulinganisha na mazao mengine ambapo mkulima au mfanyabiashara anaweza kuvuna na kuuza wakati wowote katika mwaka.

Lutego amesema kuwa kama nchi wana mkakati wa kufikisha tani 120,000 ifikapo 2025 ambapo wanahitaji wakulima zaidi na mashine za uchakataji ili kufikia malengo hayo.

Aidha, ametaja mikakati ya kufanikisha malengo hayo ni kuongeza ukubwa wa mashamba na idadi ya wakulima wa mkonge kwa kuhamisisha na kutoa elimu ya kilimo bora cha mkonge katika mikoa yote inayofaa kwa kilimo cha mkonge.

Ameongeza kuwa wamejipanga kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo,uzalishaji wa mbegu bora za mkonge, kuanzisha vituo vya uchakataji wa mkonge (decortication centres),kwa wakulima wadogo.

Lutego amesema mahitaji ya mkonge duniani ni tani 500,000 lakini zinazozalishwa kwa sasa ni 250,000 huku Tanzania ambayo ni ya kwanza kwa kuzalisha mkonge wenye ubora ikizalisha tani 56,000.

Amesema wakulima zaidi ya 12,000 wanajihusisha na kilimo hicho nchini ambapo wengi wakiwa ni wakulima wadogo wadogo. 

Amesema vituo vya uchakataji vipo katika Wilaya za Handeni, Mkinga na maeneo mengine ambako mwitikio wa wakulima wa mkonge umekuwa mkubwa.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI